Tuesday, January 1, 2013

Rambirambia za kifo cha Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kutoka watu mbalimbali…

                                                               Zitto Zuberi Kabwe

Zitto Kabwe (Mbunge Kigoma Kaskazini, Chadema)

Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii nchini kupata kipato stahili na kazi Yao. Kifo chake kimeniondolea Mtu niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania walio kwenye entertainment industry. Sajuki left an indelible mark in my politics. Pumzika Kwa Amani Juma.


EATV
BREAKING NEWS: R.I.P SAJUKI

Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.

Kwa taarifa zaidi endelea kusikiliza EAST AFRICA RADIO

Masanja Mkandamizaji
I have some bad news. Ndugu yetu SAJUKI amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina lake na lihimidiwe! Tulimpenda, tulijitahidi kufanya kile tulichoweza lakini Mungu amempenda zaidi na amemuita kwake kupumzika.! Thanks kwa support yenu kubwa sana wakati tunatafuta msaada wa matibabu yake. Mungu awabariki sana!
 
Kidojembe itaendelea kuwapa taarifa na salamu zaidi..                                               Sajuki enzi za uhai wake akiwa na afya tele...

Wastara akiwa na mumewe Juma Salim Kilowoko 'Sajuki' ndoa hii ilikumbwa na misukosuko kabla haijafungwa, na baada ya kufungwa muda mchache tu ikaendelea kupata misukosuko.

Wastara amabe ni msanii wa sanaa ya filamu nchini kama mumewe alipata ajali na kukatwa mguu lakini Sajuki hakumuacha bali alimuoa hivyohivyo...... Lakini muda mchache baada ya ndoa yao Sajuki akaanza kuugua maradhi yasiyojulikana, mpaka kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Wastara hakuvunjika moyo na aliendelea kumuuguza mumewe mpaka mwili wake ulipotengana na roho uhai ukakoma...

No comments:

Post a Comment