Wa pili kutoka kulia ama wa katikati ni Alex Kajumulo, ndie mtanzania wa kwanza kumiliki timu ya mpira akiwa mwenyewe bila shirika ama kikundi cha watu. Alivuma sana na timu ya Kajumulo baadae mambo yalipomzidia aliamua kuiuza timu hiyo na ndiyo Moro United inayoljuikana sasa.
Wa tatu kutoka kulia ni James Dandu (Marehem) alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2002 August 27 eneo la Makumbusho Dar es Salaam usiku. Ndie muasisi wa tuzo za Kili music. Atakumbukwa si kwa uwezo wake wa kuimba bali akili za kufikiria kuwapa changamoto wanamuziki wa aina zote nchini Tanzania kufanya kazi kwa juhudi ili kushindanisha kazi zao kila mwaka...
Hii ilikuwa ni siku ya kilele cha sherehe za mapinduzi mwaka huu Jan 12, 2013. Kwenye picha wanaonekana viongozi watatu waandamizi katika siasa za Zanzibar, hapa namuona Maalim Seif Sharif Hamad waziri kiongozi wa zamani na makamu wa kwanza wa Rais kwa sasa, mwengine ni aliekuwa Rais wa awamu ya tano wa Zanzibar 'Komandoo' Salmin Juma Amour, na wa tatu ni huyu alie chini anaempa mwenzie mkono ni Rais wa sasa wa Zanzibar ambae alikuwa makamu wa Rais Tanzania Dk Ali Mohammed Shein.
Hawa ni mahasimu wa kisiasa kwa vipindi tofauti, lakini leo wamekutanishwa kwa pamoja katika jukwaa moja wanacheka na kufurahi, kama hiyo haitoshi Maalim Seif anaonekana kumsaidia ama kumshika mkono Komandoo Salmin ili aweze kusalimiana na Mheshimiwa Rais, Salmin Amour anaumwa si mzee kwa maana ya utu uzima lakini ameharibika macho yake haoni vizuri.
Kido jembe inaahidi kufanyia kazi picha hizi mbili na kuandika makala nzuuuri itakayompendeza kila mmoja.
Hafidh Kido
kidojembe@gmail.com
0713 593894
15/1/2013
No comments:
Post a Comment