Tuesday, January 15, 2013

Zanzibar ni mji wa historia, ila watu wake hawajui kuuutumia ili kujiingizia kipato.

                      Hii ni shule ya uandishi wa habari Zanzibar ipo maeneo ya vuga majumba ya mawe.

 Hii ndiyo mahakama kuu ya Vuga, Unguja Zanzibar. Wenyewe wanasema ikifika siku inasikilizwa kesi ya Uamsho eneo lote linafungwa.

Hii ni Karume House, jengo lina historia kuu sana kabla na baada ya mapinduzi. Ndipo palipozinduliwa kituo cha kwanza cha televisheni ya rangi afrika mashariki na kati mwanzoni mwa miaka ya sabini baada ya kufariki Rais wa kanza wa visiwa hivyo hayati Abeid Amani Karume mwaka 1972 ambae ndie alieratibu mipango hiyo ya kuanzisha kituo cha televisheni lakini hakujaaliwa kuona matunda yake.

niliwahi kufanya kazi katika kituo hiki mwaka 2007, nilikaa miezi miwili. Karume House ama TVZ wana mashine za kisasa na ukumbi mkubwa wa kuzalisha matangazo ama kwa kizungu 'production room' ambapo kuna kila aina ya vifaa vinavyohitajika. Kuanzia taa, miamvuli ya kuleta vivuli na mashine nyingine sijui hata zinatumika vipi. Lakini havitumiki... Ajabu akidi hii...

Hafidh Kido
kidojembe@gmail.com
0713 593894
Unguja, Zanzibar

No comments:

Post a Comment