Friday, October 19, 2012

Ama kweli mpira wa Tanzania ni Yanga na Simba......


Mwandishi wa habari Shaffih Dauda ameandika kwamba kampuni ya simu za mkononi Vodacom ambao pia ni wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wamefikia muafaka na klabu ya Yanga juu ya kutotumia jezi zenye nembo nyekundu.
Vodacom imefikia hatua hiyo kutokana na Yanga kupeleka maombi yao ya kuomba kutotumia nembo hiyo nyekundu katika jezi zao, vodacom imeona ni busara kuwasikiliza Yanga hivyo kuamua kuipa nafasi ya kuchagua nembo moja kati ya hizo tatu hapo juu.

No comments:

Post a Comment