Ndugu Wananchi,
leo tarehe 12
Oktoba, 2012 ni Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa
(International Day for Disaster Reduction). Siku hii huadhimishwa tarehe 13
Oktoba ya kila mwaka. Hata hivyo, kwa mwaka huu Sekretariati ya Kupunguza
Athari za Maafa ya Umoja wa Mataifa, imeelekeza kuwa siku hii iadhimishwe leo
siku ya Ijumaa Oktoba 12, 2012. Kama ilivyo
kwa miaka yote tangu siku hiyo ilipoanzishwa katika miaka ya 1990, Sekretarieti
hiyo hutoa Kaulimbiu ya mwaka husika. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema, “WANAWAKE
NA WASICHANA – NGUVU ISIYOONEKANA KATIKA KINGA DHIDI YA MAAFA” (WOMEN AND GIRLS
–THE INVISIBLE FORCE OF RESILIENCE). Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari
za Maafa kwa mwaka huu imewalenga Wanawake na Wasichana kwa lengo la kutambua
na kukubali mchango unaotolewa katika jamii na mamilioni ya Wanawake na Wasichana
katika kukabili athari za maafa na Mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuleta
manufaa katika shughuli za maendeleo na Ndugu Wananchi, mtakubaliana na mimi
kwamba mafanikio makubwa yatokanayo na nguvu za wanawake na wasischana
hayatambuliwi kwenye shughuli za maafa na katika kufanya maamuzi kutokana na
kutokutambua mchango wao katika jamii. Kwa kulitambua hili ndiyo maana ujumbe
wa mwaka huu unasisitiza kutambua ushiriki wa 1 wanawake na wasichana katika
kulinda na kujenga jamii kabla na baada ya Maafa. Ndugu Wananchi, lengo kubwa
la kaulimbiu ya mwaka huu ni kuamsha uelewa wa wananchi katika masuala
yafuatayo:- i. Jamii kutambua mchango wa Wanawake na Wasichana kabla, wakati na
baada uwezo wa Wanawake na kutokushirikishwa katika shughuli za upunguzaji wa athari
za maafa na katika kutoa maamuzi kwenye ngazi za uongozi pamoja na mipango ya
progamu na uelewa mdogo wa jamii juu ya usawa wa jinsia; iii.Kuondokana na
mtazamo kwamba daima wanawake na wasichana ndiyo waathirika wakubwa wa maafa;
na iv. Kudhihirisha vielelezo vya shughuli na jitihada zinazofanywa na Wanawake
na Wasichana katika kukabiliana na maafa. Ndugu Wananchi, napenda nielezee
hatua chache zilizochukuliwa na Serikali yetu kuwezesha ushiriki wa wanawake
katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na shughuli za
upunguzaji athari za maafa katika ngazi za kisiasa na kutoa maamuzi kwa kuwapa
fursa ya moja kwa moja katika kusimamia Ofisi za Umma zikiwamo Wizara, Taasisi
na Idara pamoja na kutambua umuhimu wao katika uandaaji wa sera, mikakati na
mipango ya kiuchumi. Ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi wa kisiasa
mathalan, Wabunge Wanawake wameongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 1990 hadi
kufikia asilimia 36 mwaka 2011. Kwa upande wa Mawaziri waliongezeka kutoka
asilimia 12 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 27.5 mwaka 2011. Aidha, kwa mara
ya kwanza mwaka 2010 katika historia ya nchi yetu aliteuliwa Mwanawake kuwa
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania . Kwa upande wa Wakuu wa
Mikoa wameongezeka kutoka asilimia 10 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 29 mwaka
2012 wakati Wakuu wa Wilaya wameongezeka kutoka Asilimia 19 mwaka 2004 hadi
kufikia asilimia 32 mwaka 2012. 2 Kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Menejimenti
ya Maafa ya mwaka 2004, Wakuu wa Mikoa na Wilaya ndiyo Wenyeviti wa Kamati za
Maafa katika ngazi zao. Katika ngazi ya uongozi wa kiutendaji, Majaji wanawake
wameongezeka kutoka asilimia 6 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 35 mwaka 2011.
Wakurungezi wa Halmashauri wameongezeka pia kutoka asilimia 6 mwaka 1991 hadi
kufikia asilimia 26 mwaka 2011. Tukizingatia Sera yetu ya Taifa ya Menejimenti
ya Maafa ya mwaka 2004, Wakurugenzi hao ndiyo Makatibu wa Kamati za Maafa za
Wilaya zao ambazo zina majukumu ya kusimamia masuala ya maafa katika maeneo yao . Ndugu Wananchi, ili
kuamsha uelewa wa jamii kutambua na kukubali umuhimu wa wanawake na wasichana
katika kukabili na kupunguza athari za maafa na mabadiliko ya tabia nchi,
Serikali imewezesha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera na Mikakati ya
maendeleo. Lengo la hatua hii ni kufikia usawa wa jinsia kwa kuanzisha jumla ya
Madawati ya Jinsia 188 katika Wizara 26, Wakala za Serikali Saba, Sekretariati
za Mikoa 21, Halmashauri 133 na Idara inayojitegemea moja. Aidha, Serikali
imewajengea uwezo wanawake kupitia mafunzo ya fani mbalimbali yaliyofadhiliwa
na Mfuko wa Mafunzo kwa Wanawake Tanzania (TFTW). wanawake 445 waliwezeshwa
kupata mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika fani za sheria, uongozi na
utawala, mipango, sayansi na teknolojia, ushauri nasaha, ujasiriamali Vilevile,
kwa kuzingatia kuwa wanawake walikuwa wameachwa nyuma kimaendeleo
ikilinganishwa na wanaume, serikali imefanikiwa kutekeleza hatua mbalimbali za
kuwawezesha wanawake kiuchumi. Hatua hizo ni pamoja na kuanzisha na kuendesha
Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake mnamo mwaka 1993 kwa lengo la kutoa mikopo yenye
masharti nafuu kwa wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hadi sasa kiasi cha
Shilingi 2,005,234,000/- kimekopeshwa kwa wanawake 40,105 katika Halmashauri
zote 134 nchini. Aidha, katika kuwajengea wanawake na wanaume uwezo, Benki ya
Wanawake Tanzania
hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2011 ilitoa mafunzo ya ujasiriamali 3 kwa wateja
wake kabla ya kuwapatia mikopo wajasiriamali 5,246 wakiwemo wanawake 4,358 na
wanaume 888. Ndugu Wananchi, Taarifa ya Dunia ya Tathmini ya Upunguzaji Athari
za Maafa ya Mwaka 2011 (Global Assessment Report on Disaster Risk Reduction
(GAR) 2011), inabainisha kuwa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania
zinakubaliana kuwa kukosekana kwa utaalamu wa kuingiza masuala ya jinsia katika
mipango ya maendeleo imekuwa ni kikwazo kikubwa cha kinga dhidi ya maafa.
Ripoti hii imeonesha kuwa asilimia 26 ya nchi ikiwemo nchi yetu ndizo zilizotoa
taarifa ya umuhimu wa kujikita katika masuala ya jinsia kama
chachu ya maendeleo. Ndugu Wananchi, kuna vipengele vitatu katika kampeni hii
ambavyo ningependa Wizara, Taasisi na Idara za Serikali pamoja na Wadau wote wa
Maendeleo kwa kushirikiana na wananchi wavizingatie ili nguvu ya wanawake
katika kinga dhidi ya maafa ionekane. Vipengele hivi vinatokana na ujumbe
muhimu wa Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji Athari za Maafa 2012 ambavyo ni: i.
Wanawake na Wasichana Wawezeshwe kwa Usalama wa Kesho Wanawake na Wasichana
wawezeshwe katika kuchangia kuleta maendeleo endelevu kwa kupunguza athari za
maafa, hususani katika utunzaji wa mazingira na usimamizi wa mali asili,
utawala na mipango ya matumizi ya ardhi na miji pamoja mipango ya kiuchumi na
kijamii ambayo ndiyo mihimili ya kinga ya ii. Wananawake na Wasichana Nguvu Kuu
ya Mabadiliko Ili jitihada za upunguzaji wa athari za maafa ziweze kuleta
matokeo mazuri ni vyema jamii iwashirikishe Wanawake na Wasichana katika
uandaaji na utekeleji wa sera, mipango na mikakati ya kinga dhidi ya maafa.
Asilimia 52 ya watu Duniani ni Wanawake na Wasichana, kwa upande wa Tanzania ni
asilimia 51 ambao ni miongoni mwa waathirika wa maafa. Hapa nchini inakadiriwa
kwamba wanawake hasa wa Vijijini wanatoa Asilimia 80 ya 4 wafanyakazi katika
kazi hasa za mashambani na hivyo kutoa Asilimia 60 ya chakula kinachozalishwa.
Hivyo uzoefu, ujuzi na uelewa wao ni muhimu sana katika mikakati na shughuli za
Upunguzaji wa Athari za Maafa na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi. Mchango ya
Wanawake na Wasichana utakuwa na matokeo mazuri iwapo watashirikishwa katika
hatua zote za menejimenti ya maafa. iii. Jamii yenye Kinga Dhidi ya Maafa ni
Jamii Inayojali Jinsia • Kutokuwa na Usawa wa Jinsia ni Udhaifu – Kuimarisha
Usawa wa Jinsia ni Kuimarisha Kinga Dhidi ya Maafa Kutokuwa na usawa wa jinsia
unawaweka wanawake, watoto na jamii nzima katika hatari pindi majanga ya asili yanapotokea.
Kwa hali hiyo tujenge na kuboresha kinga dhidi ya maafa kwa kutoa elimu kwa
uwiano sawa wa jinsia. • Itambulike Kuwa Uwiano Sawa wa Jinsia Unaanzishwa na
Elimu Wanawake na Watoto lazima washiriki katika kufahamu jinsi ya kujiandaa,
kukabili na kupunguza athari za maafa katika jamii. Hili litawezekana kwa
kuwaelimisha wavulana na wasichana katika rika zote. Wanaume na wavulana
wakihusika wataweza kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanawake na wasichana
kushiriki katika mzingo mzima wa upunguzaji athari za maafa. na Wasichana ni
Njia sahihi ya mawasiliano ni ile inayohusisha pande mbili kwa kushirikisha
sauti za Wanawake na Wanaume katika kujiandaa, kukabili na kupunguza athari za
maafa. Hivyo, jamii itaweza kuwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya maafa na kupata
maendeleo endelevu. Ndugu Wananchi, pamoja na mambo yote haya kama tutaongeza
mkazo katika kutambua mchango unaotolewa na Wanawake na Wasichana kwa
kuwashirikisha katika kuandaa na kutekeleza shughuli za Upunguzaji wa Athari za
Maafa na kutoa maamuzi kwenye ngazi za uongozi pamoja na mipango ya progamu,
sera na mikakati tunaweza 5 kuiona nguvu ya wanawake katika kinga dhidi ya
maafa. Natoa wito kwa Viongozi wote katika Wizara, Idara, Taasisi
zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri
ziendelee kuzingatia masuala ya jinsia katika Sera na Mikakati na Mipango yao
ya maendeleo kwa lengo la kufikia usawa wa jinsia ili nguvu ya Wanawake na
Wasichana katika kinga dhidi ya maafa ionekana dhahiri kwa jamii. Ikumbukwe
kuwa, jukumu la kupunguza athari za maafa ni la jinsia zote. Kila mmoja pale
alipo atimize wajibu wake.
ASANTENISANA
Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb) WAZIRI MKUU
ASANTENI
Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb) WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment