Saturday, October 20, 2012

Dada huyooo ameolewaa.... mahaariii ishatolewaa...

Aunt Ezekiel, mwigizaji maarufu kwa kuvaa viguo vya uchokozi akisaini cheti cha ndoa ikidhihirisha amekuwa Muislam. Baada ya kufunga ndoa na tayari yupo katika mchakato wa kuelekea uarabuni kujiunga na mumewe siku yoyote kuanzia leo.

kidojembe iliwahi kuripoti juu ya sakata la dada huyu kuiomba jamii ya watanzania radhi kufuatia kuonyesha utupu katika tamasha la muziki la fiesta mjini Dodoma. Na katika maombi hayo alisema anaweza kuolewa siku za karibuni hivyo wakwe zake pia watafurahi ikiwa watanzania watamsamehe. Kumbe alikuwa hasemi uongo, ameolewa kweli....

No comments:

Post a Comment