Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Tanzania Limited, Jokate Mwegelo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa lebo yake ya Kidoti kwenye hotel ya Serena.
Na
Mwandishi wetu
Miss Tanzania namba
mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo amezindua rasmi lebo yake ya mitindo
ya nywele na nguo
ijulikanayo kwa jina la Kidoti Brand.
Jokate
ambaye alianza kujihusisha na masuala ya mitindo mwaka jana, alizindua lebo yake
hiyo kwenye hotel ya Serena na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa masuala ya
urembo, maonyesho ya mavazi, wanamitindo na wauzaji wa bidhaa hizo kutoka kila
kona ya jiji.
Alisema
kuwa hatua ya kuamua kuanzisha lebo hiyo ni moja ya mikakati yake ya kujitafutia
fedha kama mjasiliamali na lengo lake
kubwa ni kutaka kusimama
yeye mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu.
Alifafanua
kuwa kabla ya kuanzisha lebo na kampuni yake, alifanya utafiti wa hali ya juu,
kuhusiana na sekta hiyo na hatimaye kushiriki kwa mara ya kwanza katika
maonyesho ya mavazi ya Red Ribbon na sasa kuamua kwenda mbali zaidi kwa kuingia
katika fani ya nywele ambazo anatengeneza
yeye mwenyewe.
Amesema
kuwa mbali ya kushiriki katika maonyesho mbali mbali, pia atakuwa anasambaza
bidhaa zake za nywele na nguo kwenye maduka mbali mbali ili kuwawezesha
wananchi kutumia bidhaa zake.
“Lengo
langu kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea, hiyo ndiyo ndoto yangu pamoja na
kuuza bidhaa zangu hasa za nywele kuanzia shs 9,500 na 12,000. Nguo za Kidoti
zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya
urembo pamoja na vipodozi,” alisema Jokate.
Alisema
kuwa msingi wa ubunifu wake
ni mchanganyiko wa kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika pamoja na mitindo
ya kisasa ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume wa kisasa.
Chanzo: Mjengwa blog
No comments:
Post a Comment