Wednesday, October 17, 2012

Leo nami nilishiriki mdahalo wa kimaendeleo British Council....

 Prof Max Mmuya huyu, akitoa neno wakati wa kuchangia mada za kimaendeleo leo asubuhi.

 Naibu waziri wa nishati na madini George Simbachawene pia alikuwepo lakini hakuna cha maana alichozungumza.

 Prof Mmuya akiwa na mama ambae anapenda kuitwa Binti Marie Shaba ambae ndie alikuwa muongoza mada leo.

                                     Nami nilikuwepo jamani msijesema nimedanganya bure.

 Huyu ni Ernest Sungura ni mwalimu wangu wa masuala ya habari pale TSJ, lakini kwa sasa ni mtendaji mkuu wa TMF (Tanzania Media Fund) nae alikuwepo.

 Bwana Kileo mwenye tai, akizungumza na mmoja wa washiriki. Kileo alikuja kuangalia upepo wa wanahabari maana yeye ni afisa habari wa wizara ya nishati na madini.

 Waziri Chimbachawene hapa akiaga baada ya kuzungumza alichojaaliwa na kudai ana haraka.


Wanahabari hawa tena ni wanahabari nguli usifanye mchezo, wanasikiliza mada leo asubuhi.



Leo tena kidojembe nilihudhuria mdahalo mwingine wa kimaendeleo, ni kuhusiana na masuala ya msingi kuhusu uchumi wetu hasa katika mafuta na gesi rasilimali ambazo zimeanza kuimbwa na watu wote hapa nchini.

Mdahalo uliwahusu wahariri wa vyombo vya habari, lakini kwa bahati baya mhariri wangu alipata dharura akataka nikamuwakilishe, nami sikujivunga.

Mdahalo ulifanyika katika ukumbi wa British Council ulikuwa na kichwa cha habari ama Theme iliyosema ‘Natural Resource Boom, Corruption and state capture in Africa. How Tanzania can unleash its potential growth sa a pole for East Africa’s Growth’. Mdahalo huu uliandaliwa na asasi ya Agenda Participation 2000.

Siwezi kuandika kila kitu nilichosikia katika mdahalo ule maana haukuwa mrefu na wahariri hawakupata muda wa kujimwagamwaga vya kutosha. Lakini nilifurahishwa na wageni wawili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mmoja kutoka kitivo cha biashara na mwingine kitivo cha sayansi ya jamii ambae amebobea katika sayansi ya siasa.

Prof Max Mmuya, ni msomi wa sayansi ya siasa, na ameandika vitabu vingi sana kuhusiana na siasa ya Tanzania. Tatizo alilogundua katika siasa ya mafuta na kusimamia rasilimali ni uongozi mbovu.

Alitoa mfano wa kuchekesha wa ‘bodaboda culture’ yaani alifananisha utawala wetu na waendesha pikipiki maarufu bodaboda, maana kwa maelezo yake aliwaona hawafuati sheria wala taratibu za barabara. Ndivyo walivyo viongozi wetu.

Nami nilipopata nafasi nilitoa dukuduku langu kwa kutolea mfano wa viongozi ambao hawatakiwi kuwa wa kisiasa, lakini Serikali kwa kuwa inaongozwa na viongozi wala rushwa wale watu ambao hawakutakiwa kuendeshwa na siasa kwa sasa ndiwo wanaofanikisha maovu ya wanasiasa.

Kwa mfano wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu wakuu wa wizara na maafisa wengine wa serikali pamoja na wakurugenzi wa mikoa na wilaya. Hawa hawatakiwi kuwa wanasiasa, lakini kwakuwa viongozi wetu wana maslahi katika nafasi hizo hupendelea kuwaweka watu wao ambao baadae watakuwa wanatenda yale wanayowaambia.

Kwa namna hii rasilimali zetu haziwezi kuwa salama hata kidogo, ikiwa jaji mkuu, mwanasheria mkuu na wengine wa aina hiyo hawafanyi kazi zao kutokana na taaluma bali wanaangalia yule aliewateua anawaambia nini.

Nae Dk Camillus Kassala, kutoka taasisi ya usimamizi wa fedha alisema hakubaliani na utaratibu wan chi kwa sasa kwani tunayo mikakati ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 kuna mahala lazima tufike, ila hakuna hata kimoja kinachotekelezwa kuhakikisha tunafika huko.

Alitoa mfano wa neon PESTEL na kusema P- Political, E- Economical, S- Social, T- Technological, E- Environmental na L- Legal.

Vitu hivyo ndivyo vya msingi kuvifuata ikiwa tunataka kuendelea, lazima tuwe na siasa safi, uchumi imara, jamii inayijitambua, teknolojia inayofuata mabadiliko ya dunia, pia tuangalie maendeleo yetu hayaharibu mazingira kwa kuwa kizazi kijacho kinahitaji urithi pia akamalizia kuwa lazima utawala wa sheria uwepo.

Mwisho kabisa Dk Kassala alituacha na kibwagizo kimoja kwa kusema ‘In the world there is things which are Logical and not always Practical, and Practical are not always Right, any thing Right are not always Ethical, anything Ethical are not always Desired, anything Desired are not always Logical”

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
17/10/2012 

No comments:

Post a Comment