Wednesday, October 17, 2012

JK atunukiwa nishani ya juu ya heshima na Sultan Qaboos...

 Sultani wa Oman, Qaboos bin Said Al Said (kulia)  akimtunuku Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman.

Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyabiashara wa Oman na Tanzania waliohudhuria Mkutano Maalum wa wawekezaji Tanzania uliofanyika jijini Mascat Oman usiku wa kuamkia jana. Mkutano huo wa wawekezaji ulihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe,Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda, Waziri wa Kazi Ushirika na Uwezeshaji Kiuchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Haroun Ally Suleleiman, Naibu Waziri waFedha na Uchumi Janet Mbene na viongozi waandamizi mbalimbali wa serikali zote mbili.


 Hapa Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi wa Oman juu ya ushirikiano na Tanzania kibiashara...No comments:

Post a Comment