Bazoka akipiga msondo dakika zote 90, mpaka Wekundu wa Msimbazi wakawa kimyaaa... ingawa tulitoka suluhu ya bila kufungana.
Huyu nae alikuwepo, mtazame vizuri kama unamjua.
Juma Pondamali 'Mensah' akiwafua magolikipa wa Coastal kabla ya mchezo kuanza....
Pius akiimba kwa hisia huku mashabiki wakiitikia kama wapo kwenye zafa vile. Inatia raha sana.
Kidojembe nami sikuwa nyuma.
Wakati watu wananunua fulana za Simba na Coastal, wapo waliokuwa wakinunua fulana za Yanga.
Chalaluza, aliesimama juu mwenye kofia kijana maarufu Mkoani Tanga, mwenyewe anasema tangu uwanja wa Mkwakwani ujengwe hajawahi kuingia kwa kiingilio.
Vijana wa coastal wakiingia uwanjani huku wakiongozwa na gari ya mwenyekiti Hemed Aurora.
Washabiki wa Simba hawa...
Umeona kikundi chote hicho? Hao ni viongozi wa simba wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu pembeni namuona Hassan Asanoo Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa pwani. Washabiki wa coastal tulikuwa wawili tu mimi na mwalimu Eddy Shossy. Tulipanda gari ya Kaburu, ilikuwa furaha sana njiani kucheka na kutaniana. Ama kweli Coastal na Simba ni ndugu ila nikamwambia Kaburu, tukiwa uwanjani tunakuwa maadui akacheka sana. Hapa tulishuka kuchimba dawa maeneo ya Chalinze, Noah ya Kaburu hakika ilitusaidia maana mara baada ya mechi kumalizika tukaingia barabarani mpaka saa sita na nusu ya usiku tupo Magomeni.
Umeamini kuwa simba na Coastal ni ndugu? Wakati tunakwenda Tanga jana asubuhi tulipanda Simba mtoto Bus. Tulikuwa na Makamu Mwenyekiti wa Coastal 'mwenye kofia' na wa mwanza kushoto ni mshabiki wa Simba damu hao wa katikati ni Coastal damu. Na tuliporudi tulipanda gari moja na makamu mwenyekiti wa Simba, raha eennhh?
Uwanjani vijana wa coastal walitandaza soka la uhakika hata baada ya mshambuliaji wao Nsa Job kupewa kadi nyekundu lakini vijana hawakuonyesha kutetereka.
No comments:
Post a Comment