Friday, October 19, 2012

Ndugu zangu nilipofika magomeni nilishitushwa sana na hali ya ukimya...
 Hapa ni maeneo ya magomeni mapipa karibu na msikiti wa kichangani. Na huu ni mgahawa wa Basmat ambao muda kama huu wa mchana unajaa watu lakini kama unavyoiona.

 Waislam wakitokwa na machozi baada ya kupigwa mabomu na askari wa FFU.
 Askari wa kutuliza ghasia FFU wakihakikisha waislamu katika msikiti wa kichangani ambao inaripotiwa walimpiga imamu wao msaidizi Sheikh Omar Walid Alhad, ambae aliwaasa Waislm wenzie wasiandamane badala yake watumie hekima. Lakini walimpiga vibaya na kukimbizwa hospitali ya Muhimbili na watu wa usalama.


Hawa unaowaona ni wanajeshi wa JWTZ ambapo ni mara chache sana kuitwa kuja kutuliza ghasia.

No comments:

Post a Comment