Sunday, October 7, 2012

Habari picha, mchezo wa jana ligi kuu bara Coastal Union dhidi ya Ruvu shooting jana....

 Kocha mpya wa Wagosi wa kaya Mohammed Moroko, akiwaeleza kitu wachezaji wake baada ya kuchapwa goli mbili kipindi cha kwanza. Magoli yaliyodumu mpaka dakika ya 90. Coastal 0- 2 Ruvu Shooting.

 Chuse na Tip wakiwa na majonzi baada ya kuona furaha yao imeingia doa. Si mchezo unatoka Tanga unakuja mkoa wa pwani unarudi kwa aibu. Chuse (alieshika tama) alikuwa ni miongoni mwa mashabiki waliokuwemo kwenye gari ya Mwenyekiti wa Coastal Hemed Aurora iliyopata ajali eneo la Mbwewe wakirudi Tanga usiku. Ila hakuna aliepata madhara makubwa zaidi ya mwenyekiti kuumia kidogo pamoja na mdau mwengine ndugu Abdi Masamaki alieumia goti.


 Bin Wandi (anaeimba) akiongoza kigoma cha Coastal kuinua hamasa ya mchezo. Wandi alizima kigoma dakika ya 60 ya mchezo na kuondoka uwanjani kwa hasira.

 Jembe nikiwa na ndugu zangu mambo si mazuri jamani, hapa kuna ndugu watatu Chuse (alieshika tama) ni mtoto wa mama mkubwa, na Tip (aliesimama) ni mtoto wa shangazi. Hivyo sote ni ndugu hapo.


 Nikiwa na Abdul maarufu Abdul Chogo, wakati wa kurudi jamaa kanuna huyo haamini kama tumefungwa.

                              Danny siku hiyo hakuonyesha ule uwezo niliozoea kuuona kwake.


                        Bench la wachezaji wa Coastal wakiwa na majonzi hawaamini kinachoendelea.

 Mwenyekiti wa Coastal Hemed Aurora (alietia mikono mfukoni), akipokea lawama kutoka kwa mashabiki wenye hasira (hawapo pichani) juu ya mwenendo mbaya wa timu na viongozi waliokabidhiwa timu na kukaa nayo kwa siku tatu katika mji wa kibaha.

 Wanachama wakiwa wanajadiliana wakati wa mapumziko. Zilikuwepo fununu za hujuma na wachezaji kulazwa hoteli ya hadhi ya chini tena bila ya usimamizi maalum. Wapo waliolewa pombe na wapo waliolala na wanawake. Na ndiyo maana wachezaji walionekana kuchoka sana hata kufungwa goli mbili bla majibu.


                                                                  Mjadala unaendelea.

Eddy Shossy mdau mkubwa wa Coastal alikuwa akizungumza kwa hasira juu ya mwenendo mbaya wa timu.
Kumbukeni tulicheza game hiyo katika uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi Mkoa wa Pwani. Wakati wa kurudi nikiwa nimechoka na hasira nyingi nikakutana na balaa jingine. kwenye daladala kulikuwa na mifugo.

No comments:

Post a Comment