Saturday, October 20, 2012

Wanajeshi walikuwa wanatoka Lugalo wanakwenda kutuliza ghasia mjini.... Fuata kilichotokea maeneo ya Tabata.....

                                               Kwanza waliwekwa sana kwenye foleni....

 Uzalendo ulipowashinda wakaamua kumtafuta trafik aliehusika kuwaweka sana kwenye foleni ya magari.

 Wananchi wakaanza kuvutiwa na picha hiyo ya bure wakakusanyika kuona kitakachofuata.

Ilibidi hekima itumike kumaliza ubishi huo, maana badala ya FFU kutuliza vurugu za Waislam wangekuja kutuliza vurugu za trafik na wanajeshi.


Wanajeshi wanaokadiriwa kuwa 50 kwa pamoja wamemshambulia trafiki kwenye taa za ubungo na kuondoka kwa madai kuwa kawachelewesha kwenye foleni, baada ya kuondoka magari hayo ya jeshi yalizuiwa kwa muda wa zaidi ya saa moja maeneo ya Tabata dampo. kabla ya kuachiwa kuendelea na safari yake.

Picha na Mjengwablog

No comments:

Post a Comment