Thursday, October 18, 2012

Rais JK apangua safu ya uongozi TBC....


Na Veronica Kazimoto – MAELEZO Dar es Salaam 18.10.2012.
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amemteua Prof. Mwajabu Possi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 8 Octoba, 2012. Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewateua wajumbe mbalimbali wa bodi hiyo ambao ni Dkt Mariam Nchimbi, Gideoni Mbalase, Prof. Elizabeth Kiondo na Balozi Kassim Mwawando. Wajumbe wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Zanzibar Omary Chunda pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Clement Mshana. Wakati huo huo Waziri Mkangara amemteua Christopher Gachuma kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya. Aidha amewateua Pendo Malebeja, William Erio, Richard Ndassa, Lina Kessi, Leornard Thadeo na Allen Alex kuwa wajumbe wa bodi hiyo.

No comments:

Post a Comment