Saturday, October 20, 2012

Taarifa zilizotufikia hivi punde.....


 Kikundi cha UAMSHO mjini Zanzibar kimesema Kiongozi huyo amepatikana hai usiku wa kuamkia leo. kabla uamsho waliipa serikali masaa 26 hadi leo alasiri amiri wao awe amepatikana vinginevyo hali itakuwa mbaya.

UAMSHO ni kikundi cha kiislam kinachodai haki ya kujitenga kwa Tanganyika na Zanzibar kwa madai muungano unawaharibia utamaduni wao. Wiki iliyopita kiongozi huyo Sheikh Farid Ahmed (pichani) aliripotiwa kutekwa nyara na watu wa usalama wa taifa hivyo kufanya kutokea vurugu kwabwa baina ya serikali na waislam mjini humo.

Vurugu hizo zilizosababisha kifo cha askari mmoja wa FFU, CPL Said Abdulrahman pamoja na mwananchi mmoja Salum Muhoja.  

No comments:

Post a Comment