Thursday, October 25, 2012

Mawakili wa Uamsho wajitoa kuwatetea wanauamsho kutokana na usumbufu wanaofanyiwa na mahakama.


 Huyu ni Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita waliopelekwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi na kuhatarisha amani katika nchi.

                                                     Mahakama Kuu ya Zanzibar.
  
Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma na Salim Tawfik walizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na usumbufu wanaofanyiwa wateja wao  kuhangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafaka.Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment