Monday, October 15, 2012

Msanii wa Bongo Movie Aunt Ezekiel aomba radhi kwa kuonyesha kufuli yake hadharani....




 Aunt Ezekiel akionekana mwenye majuto wakati akizungumza na wanahabari leo asubuhi katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO.

 Waandishi wakiwa makini kuhakikisha hawakosi picha hata moja ya Aunt.....

 Hapa akiwa katika harakati za kuhakikisha hijabu yake haimtiki kichwani, wapo waandishi waliozungumza na kidojembe pembeni na kudai Aunt hajazoea kuvaa ushungi anafanya hivyo kulinda uchumba wake utakaozaa ndoa mwezi ujao. Pia inadaiwa Aunt amebedili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu ili aolewe.... mhhhh kidojembe nilikuwa sijui...


 Hapa akionekana na msanii wmenzie Tino, akijitahidi kuwashawishi wanahabari kupiga picha vizuri ili jamii isiwahukumu wasanii kwa kuvaa vibaya.

 Hapa katibu wa shirikisho la filamu Tanzania Wilson Mwakune, akijitahidi kumuombea radhi Aunt huku mwenyewe akionekana pembeni kama anajutia kitendo chake.

Ahahahaa hii habari ya Aunt Ezekiel na Wema Sepetu iliwavutia wanahabari wengi sana, mpaka Kambi Mbwana wa Mtanzania na Bingwa pia alikuwepo. Huwa haji sana hapa MAELEZO, kijiwe cha wasanii wa Dar es Salaam na Tanzania.


Na Hafidh Kido

Mwigizaji wa filamu za kitanzania maarufu Bongo Movie, Aunt Ezekiel amejitokeza mbele ya jamii na kuomba radhi juu ya kitendo cha kuonyesha nguo za ndani katika tamasha la muziki lililofanyika mjini Dodoma.

Akizungumza na waandihsi wa habari leo asubuhi mjini Dar es Salaam, Aunt Ezekiel ambae alitakiwa kuandamana na msanii mwenzie walioshiriki pamoja katika tamasha hilo la Fiesta Wema Sepetu ambae hakufika kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi alisema anaiomba radhi jamii ya watanzania kwani ilikuwa mara yao ya kwanza kushiriki tamasha lile na hakujua urefu wa jukwaa na aina ya mavazi yatakayoweza kuwasitiri maungo yao tofauti na wasanii wa kike wa muziki ambao walionekana kutambua matamasha hayo hivyo kuweza kujisitiri vizuri.

“Unajua ile ni mara yetu ya kwanza wasanii wa Bongo Movie kushirikishwa katika tamasha la Fiesta, hivyo hatukujua kama majukwaa yanayotumiaka ni marefu sana kiasi mtu akiwa chini anaweza kuona nguo yako ya ndani na kukufanya uonekane muhuni wakati sivyo ilivyo,” alisema Aunt Ezekiel kwa huzuni.

Hata hivyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa Habari Ezekiel alionekana kubabaika baada ya Kidojembe kumuuliza kuwa anakunywa pombe na  kujikuta anakiri mbele ya wanahabari kuwa alikuwa amekunywa pombe siku ya tukio hivyo kutotambua alichokifanya. Lakini baada ya kuulizwa na Hemed Kivuyo kutoka Radio One, juu ya hali ya ulevi Aunt Ezekiel alipinga kusema alikuwa amelewa.

“Naomba ieleweke, niliulizwa hapa kama nakunywa nikajibu nakunywa, na nilipoulizwa tena kuwa siku ya tukio nilikunywa nikakiri nilikunywa lakini hakuna mahali niliposema nimelewa. Nakiri siku hiyo nilikunywa lakini sikuwa nimelewa,” alisisitiza Aunt.

“Ndugu waandihsi wa habari pamoja na yaliyotokea tunachukua fursa hii kuomba msamaha kwa wizara ya habari utamaduni na michezo, shirikisho la filamu Tanzania, Bongo Movie Club na wadau wake, familia zetu na jamii kwa ujumla kutokana na picha zilizopigwa tukiwa katka tamasha la Fiesta mjini Dodoma ambazo zimesambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” aliongeza Aunt Ezekiel kwa niaba ya msanii mwenzie Wema Sepetu.

Hata hivyo mwigizaji huyo maarufu kwa kuvaa viguo vifupi aliweka wazi kuwa hatoacha kuvaa viguo vifupi ingawa hatofanya hivyo katika hadhara bali atakuwa anaonyesha akiwa katika filamu tu.

“Mimi ni mwigizaji, zipo aina ya filamu zinakutaka kuvaa nguo fupi siwezi kuacha lazima nifuate agizo la mwongozaji filamu hii ni kazi yangu. Naomba msamaha katika jamii lakini naomba niweke wazi kuwa sitoacha kuvaa nguo fupi,” Aunt.

Wakati akimalizia mkutano huo katibu wa shirikisho la filamu Tanzania Wilson Mwakume, alisema kuwa Aunt Ezekiel amekwazwa sana na tukio hilo hasa ikizingatiwa mwezi ujao anategemea kufunga ndoa na mchumba wake, hivyo familia ya mchumba wake imejisikia vibaya baada ya kuona picha zile katika vyombo vya habari. Na shirikisho lao lilipokaa katika kikao cha nidhamu waliwaita wasanii hao na kuwataka waiombe radhi jamii na kuahidi kutorudia kitendo hicho cha aibu.

HAFIDH KIDO

DAR ES SALAAM, TANZANIA


0713 593894/ 0752 593894

15/10/2012

 

No comments:

Post a Comment