Friday, October 5, 2012

Leo ndiyo nimekamilisha kozi fupi ya siku mbili juu ya namna ya waandishi kujilinda wakati akiwa katika matukio ya hatari kama vita, maandamano, moto, ama mwandishi akitekwa ama akiwa anawindwa na wabaya...

 Nikiwa na jembe langu Evans Magege wa Mtanzania, tulikuwa waandishi takriban 16 kutoka vyombo mbalimbali Tanzania..

 Hivi ndivyo cheti cha jembe lenu kinavyoonekana, naweza kupata kazi? Maana watanzania tunasoma ili kupata kazi ama nakosea?


 Leo tulifundishwa namna ya kujipa huduma ya kwanza ikiwa utakuwa katika sehemu ya hatari. Huyu ni mkufunzi Maulid Kapiteni kutoka Tanzania Red Cross. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kumjulisha mwanahabari vipi atajua haya ni mazingira hatari ama akiwa na wenzake na wamepata majeraha atawasaidia vipi...

                                    Table manners was order of the day during the lunch today....

 Huyu anaitwa bwana William Oloo, ni mwakilishi kutoka Kenya katika chama cha wanahabari wa Afrika Mashariki (EAJA). Hapa akizungumza chochote kwa wanahabari wenzie.

                           Hivi ndivyo jina langu lilivyotoklezea katika karatasi ya utambulisho katika semina.

 Hapa nikiwa na mwanahabari kutoka nchini Senegal ambae alikuja kuwakilisha (IFJ) bwana Sadibou Marong. Hii ndiyo raha ya wanahabari kukutana mnabadilishana mawazo na mawasiliano.

                                          The moment of certification awards...............

Chakula halikuwa tatizo siku ya leo kikubwa ilikuwa ni kuangalia tumbo lako lina uwezo gani katika kupakia.

Mungu akipenda kesho nikipata muda wa kutosha nitaandika mambo mengi juu ya elimu hii, ni muhimu sana si kwa wanahabari tu bali hata watu wa kawaida kufahamu namna ya kujilinda. Nitakaa chini vizuuuri na niandike... stay tuned don't press the button.

No comments:

Post a Comment