Na: Mwandishi Maalum
Kwa mara ya
kwanza, jana Alhamisi, Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto
wa Kike kwa kutoa wito wa kukomesha ndoa za utotoni. Na kuhimiza elimu kama mkakati wa kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mila
hii potofu ya kuwaoza wakingali bado wadogo. Katika salamu zake katika
maadhimisho hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesmea “ elimu
kwa watoto wa kike ni moja ya mkakati wa kuwalinda dhidi ya ndoa za utotoni.
Watoto wakike
wakipata na fursa ya kukaa shuleni na kuepuka kuolewa mapema, wanajijengea
uwezo na misingi ya kuwa na maisha bora kwao wenyewe na familia zao”. Akaongeza
kwa kusema “ Hebu na tutimize wajibu wetu wa kuwaacha watoto wa kike wawe
watoto wakike na sio wachumba”. Huku akizihimiza serikali, jamii, viongozi wa
dini, vyama vya kijamii, sekta binafsi ,familia na hususani wanaume na wavulana
kutetea haki za watoto wa kike.
Mwezi wa Desemba
mwaka 2011, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio linaloitangaza
Octoba 11 ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, dhumuni likiwa
katika kutambua changamoto za msingi zinazomkabili mtoto wa kike duniani kote.
Maudhui ya mwaka huu ya siku hii ya kimataifa ya mtoto wa kike ni “Utokomezaji
wa ndoa za utotoni” Kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa, inakadiriwa
kwamba leo hii kuna wanawake vijana zaidi ya milioni 70 walioolewa wakiwa chini
ya miaka 18.
Kielelezo
kinachodhihirisha kwamba ndoa za utotoni zinamnyima na kumkatisha mtoto wa kike
haki yake ya kupata elimu, na kupunguza fursa mbalimbali na kuongeza hatari ya
kuwa mhanga wa vitendo vya kikatili na uharibifu wa afya yake. Katika
maadhimisho hayo, ilielezwa bayana kwamba mtoto wa kike mwenye elimu duni
anayonafasi kubwa ya kuolewa mapema na ndoa za utotoni zimedhihiria kuwa mwisho
wa fursa ya elimu kwa mtoto wa kike.
Aidha takwimu za
Umoja wa Mataifa zimedhihirisha pia kwamba kwa wasichana ambao wamepata fursa
ya kufikia elimu ya sekondari hawamo katika hatari ya kuolewa wakiwa na umri
mdogo na hivyo kuthibitisha kwamba elimu ndio silaha sahihi ya kupambana na
ndoa za umri mdogo.
Maadhimisho hayo hapa
Umoja wa Mataifa yamefanyika sambamba na majadiliano yaliyohusisha viongozi
mbalimbali akiwamo Askofu Mkuu Desmond Tutu na wawakilishi katoka Mashirika ya
Umoja wa mataifa ya UNFPA, UNICEF, UN Women pamoja na maonesho ya picha
zilizokuwa na maudhui “ bado ni mdogo mno kuolewa”.
Aidha maadhimisho
hayo ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, yamefanyika ikiwa ni takribani kama
siku mbili hivi kupita tangu kuuawa kwa Malala Yousufzai, msichana wa miaka 14
huko Pakistani kosa lake likiwa ni kupigania haki ya mtoto wa kike kwenda
shule, msichana huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa ni wa kundi
la Talban wakati akitoka shule.
Kifo cha msichana
huyo kimemfanya Katibu Mkuu Ban Ki Moon kuonyesha mshangao wake mkubwa dhidi ya
kiwango cha matumzi ya nguvu, vurugu, ubaguzi na unyanyasaji ambao bado
unaendelea katika karne ya leo dhidi ya mtoto wa kike.
Akasema Ban Ki
Moon, “ Kumshambulia mtoto huyo mtetezi wa haki ya wasichana kupata elimu ni
kitendo siyo tu cha udhalimu bali ni uoga wakijinga ulioonyeshwa na magaidi
dhidi ya nguvu ya elimu kwa mtoto wa kike.
Haiingi akilini mahali
popote duniani ambako kitendo cha mtoto wa kike kupigania fursa na haki yake ya
kupata elimu kikatafsiriwa kama kitendo cha
ushajaa na kusababisha kukatisha uhai wake ”.
No comments:
Post a Comment