Wednesday, October 17, 2012

Mrejesho wa kijana kunajisi kitabu cha Mungu leo vurugu zarindima tena baada ya Sheikh Ponda Issa Ponda kukamatwa...


Kamanda wa Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova akizungumza na wanahabari juu ya kukamatwa kwa Sheikh Ponda jana usiku.



 Picha hizi ni wale waliodaiwa kuwa ni waislam walioandamana wiki iliyopita kupinga kunajisiwa kitabu cha Mungu. Hapa wakisubiri karandinga kupelekwa mahabusu baada ya kesi yao kutajwa jana katika mahakama ya Kisutu.

 Huyu ndie Sheikh Ponda Issa Ponda aliekamatwa jana usiku ambapo na yeye anatarajiwa kufikishwa mahakamani. Lakini leo mchana watu waliodaiwa ni Waislamu walivamia kituo kikuu cha polisi Central na kushinikiza jeshi la Polisi kumuachia huru sheikh huyo.

Huyu ni miongoni mwa waliokuwa wakishinikiza jeshi la Polisi kumuachia huru Sheikh Ponda leo mchana kituo kikuu cha polisi. Lakini alidhibitiwa vilivyo.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ambapo amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine Sheikh huyo anahusishwa na kundi lililovaamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA pamoja na kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.


Akifafanua namna walivyomkamata Sheikh huyo kamanda Kova alieleza kuwa wamemkamata wakati akienda kwenye mafichoyake muda mfupi tu baada ya kushushwa kwenye pikipiki kwenyeeneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam.


Mbali na kukamatwa Kiongozi huyo pia watu wengine 38 wamekamatwa majira ya saa 4:00 usiku baada ya kufanya operesheni maalum. Watu hao wanakamatwa kwa madaikuwa ni wafuasi wa sheikh Ponda aliongoza kundi hilo kuvamia kiwanja No.311/3/4BLOCK "T"  eneo la Chang'ombe Manispaa ya Temeke.


 Kwenye Taarifa ya Kova kumeelezwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kusababisha vurugu na vitisho,
Sambamba na hilo Ponda na wafuasi wake anatuhumiwa pia kinyume cha sheria walisababisha kuvunjwa kwa makanisa zaidi ya manane siku ya 12/10/2012.


Hata hivyo leo katika jiji la Dar es Salaam kumekuwa na patashika katika ya polisi wa kutuliza ghasia baina ya waandamanaji waliokuwa wakitaka Sheikh huyo kuachiwa pamoja waumini wengine wanaoshikiliwa.


 Chanzo: Said Powa Blog na Mjengwa Blog.






No comments:

Post a Comment