Hizi ndizo tuzo zenyewe walizopewa na AIB International kuthibitisha ubora wa bidhaa za Pepsi.
Kutoka kushoto ni Michael Mafwenga meneja wa ubora wa viwango Pepsi na Separatus Kagashani ambae ni meneja wa kusimamia viwango vya ubora Pepsi, wakijivunia kazi yao. Maana hawa ndiwo wanaothibitisha ladha ya vinywaji vya Pepsi kabla havijaingia sokoni.
Hapa ndugu Nyirenda akisisitiza jambo kwa wanahabari wakati wa maswali na majibu.
Na Hafidh Kido
Kampuni ya SBC Tanzania
Limited wazalishaji wa kinywaji cha pepsi wametoa pongezi kwa wapenzi wa
kinywaji hicho kwa kuwaunga mkono mpaka kuweza kupata tuzo nne za kimaifa za
ubora na usalama zinazotolewa na AIB International.
Akizungumza na waandishi wa
habari makao makuu ya bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam, mkuu wa masuala ya
mahusiano SBC Tanzania Limited Foti Gwebe-Nyirenda, alisema kampuni yao imeweza kufikia hatua
hiyo kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa wanywaji na wauzaji
wa bishaa za Pepsi.
“Tunaahidi kuendelea kuwapa
wanywaji na wateja wetu waaminifu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa wakati
wote ili kuhakikisha wanaendelea kuthamini tuzo tuliyoipata kwa mwaka huu kwani
ni heshima kubwa kwetu.
“Kampuni ya pepsi ipo dunia
nzima hivyo Tanzania
kuweza kushinda tuzo nne za kimataifa hiyo ni hatua kubwa na ya kuheshimika
kuliko kawaida,” alisema Nyirenda.
Aidha SBC Tanzania Limited
inayozalisha vinywaji vya Pepsi, Mountain Dew, Mirinda Orange, Mirinda Fruity,
7up na Evervess ilipata tuzo hiyo katika mkutano wa kimataifa uliofanyika
nchini Dubai mwezi Agost 2012, katika nyanja za Utunzaji wa viwango vya ubora
katika kuhifadhi bidhaa na kuwa miongoni mwa makampuni ya Pepsi duniani
iliyofikia viwango vya juu katika Asia, Mashariki ya kati na ukanda wa Afrika.
Vilevile imeweza kutambuliwa
katika tuzo ya kampuni bora inayotoa bidhaa bora kwa mwaka 2012 baada ya
kufanyika ukaguzi na kampuni inayoongoza duniani kwa ukaguzi wa ubora ya AIB
International.
Kampuni ya Pepsi imekuwepo
nchini Tanzania
kwa kipindi kirefu na kuweza kuendelea kutoa huduma ya vinywaji laini ambapo
kwa sasa ndiyo inayoongoza barani Afrika kwa ubora wa bidhaa zake.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM , TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
11/10/2012
No comments:
Post a Comment