Na Daniel Mbega
CHINI ya miti ya
mikaratusi, kando ya Mto Mlowa, vijana wanaonekana wakijaza nyanya kwenye
matenga ya mbao huku pembeni yao kukiwa na
malundo makubwa ya zao hilo .
“Hii ni hasara kubwa,
nimekuja na matenga hamsini, lakini inaonekana yametoka thelathini tu, haya
malundo yote ni nyanya zilizolainika (masalo) ambazo haziwezi kwenda mahali
popote,” anasema Jacob Kamota, mkulima wa nyanya kutoka Kijiji cha Iyayi, Kata
ya Image wilayani Kilolo.
Jacob analalamika
kwamba, huko shambani pia ameacha malundo ya nyanya zisizofaa kusafirishwa,
ingawa zinafaa kwa matumizi ya nyumbani au hata kwa kusindikwa, hali ambayo
inazidi kumtia umaskini badala ya kujikwamua kiuchumi.
“Sina mahali pa
kuzipeleka, laiti kungekuwepo na kiwanda ningeweza kuuza nyanya zote na kupata
faida, lakini sasa hata gharama zangu sidhani kama
zinaweza kurudi,” anasema.
Chanzo: Mjengwa Blog
No comments:
Post a Comment