Thursday, October 25, 2012

Ndugai atoa ufafanuzikuhusu ripoti ya bunge...


Na Rodrick Minja,Dodoma
RIPOTI ya bunge kuhusu tuhuma za wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa,inatarajia kuwasilishwa bunge wiki lijalo. Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Spika wa bunge Anne Makinda atatoa utaratibu wa namna ya kuwasilisha ripoti hiyo ndani ya ukumbi wa bunge. Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa kwa mujibu wa Kanuni za bunge toleop la 2007, vifungu 114(17), na 119 (1) hadi (6) kwa pamoja vinampa madaraka spika kuhusu utaratibu wa kufuata katika uwasilishaji wa taarifa bungeni. “Ambapo, yaweza kuwa spika akatoa uamuzi ama kamati kuwasilisha taarifa hiyo bungeni au vinginevyo lakini spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi huo bungeni wakati wa mkutano wa tisa wa bunge unaotarajia kuanza oktoba 30 mwaka huu,” alisema Ndugai. Katika mkutano wa nane wa bunge lililopita, Spika wa bunge Anne Makinda aliunda kamati ya kuchunguza tuhuma za wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini kuhusu kujihusisha na vitendo vya rushwa. Makinda alifia uamuzi huo kufuatia tuhuma zilizokuw zimezagaa karibu nchi nzima kuwa wabunge hao wamekuwa wakijihusisha na rushwa lakini wakiwa bungeni Mbunge wa Nkasi Ali Keissy Mohamed ndiye aliyeanzisha chokonoko hizo kabla ya wabunge wengine kuidandia ajenda hiyo. Kamati iliyoundwa na spika ilikuwa chini ya Mbunge wa Mlalo Hassan Ngwilizi ambaye alisaidiwa na wajumbe Said Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki),Godbless Blandes (Karagwe) pamoja na Mbunge wea Viti Maalumu Ridhiki Juma. Kwa mujibu wa Ndugai, Kamati hiyo ilimaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa spika tangu Septemba 20 mwaka huu ambapo ndiyo siku ilipokabidhiwa kwa spika. Kwa upande mwingine Naibu spika alikemea vitendo vya baadhi ya watu na vyombo vya habari kuendelea kuanaidka na kuchapisha juu ya kilichomo ndani ya ripoti hiyo kwa maelezo kuwa ni kosa. “Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyokatika vyombo vya habari ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge kw mujibu w kifungu cha 31 (1) (g) cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya bunge sura 296,” alisisitiza Ndugai. Alifafanua kuwa kifungu hicho kinakata mtu yeyote kuchambua taarifa ya kamati kabla ya taarifa hiyo kuwasilishwa bungeni. Naibu Spika alieleza kuwa ikibainika kuwa taarifa imechapishwa wahusika wanaweza kulipa faini isiyozidi Sh 500,0000 au kifungu kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Chanzo: Mjengwa blog

No comments:

Post a Comment