Saturday, October 27, 2012

Read this....



Misconception: Why do Muslims slaughter the animal in a ruthless manner by torturing it and slowly and painfully killing it?

The Islamic method of slaughtering animals, known as Zabiha has been the object of much criticism from a large number of people.

Before I reply to the question, let me relate an incidence about a discussion between a Sikh and a Muslim regarding animal slaughter.

Once a Sikh asked a Muslim, "Why do you slaughter the animal painfully by cutting the throat instead of the way we do with one stroke i.e. jhatka?" The Muslim replied"We are brave and courageous and attack from the front. We are marad ka baccha (macho men), you are cowards and attack from behind".

Jokes apart, one may consider the following points, which prove that the Zabiha method is not only humane but also scientifically the best:
1. Islamic method of slaughtering animal
Zakkaytum is a verb derived from the root word Zakah (to purify). Its infinitive is Tazkiyah which means purification. The Islamic mode of slaughtering an animal requires the following conditions to be met:

a. Animal should be slaughtered with sharp object (knife)

The animal has to be slaughtered with a sharp object (knife) and in a fast way so that the pain of slaughter is minimised.

b. Cut wind pipe, throat and vessels of neck

Zabiha is an Arabic word which means ‘slaughtered’. The ‘slaughtering’ is to be done by cutting the throat, windpipe and the blood vessels in the neck causing the animal’s death without cutting the spinal cord.

c. Blood should be drained

The blood has to be drained completely before the head is removed. The purpose is to drain out most of the blood which would serve as a good culture medium for micro organisms. The spinal cord must not be cut because the nerve fibres to the heart could be damaged during the process causing cardiac arrest, stagnating the blood in the blood vessels.
2. Blood is a good medium for germs and bacteria

Blood is a good media of germs, bacteria, toxins, etc. Therefore the Muslim way of slaughtering is more hygienic as most of the blood containing germs, bacteria, toxins, etc. that are the cause of several diseases are eliminated.
3. Meat remains fresh for a longer time

Meat slaughtered by Islamic way remains fresh for a longer time due to deficiency of blood in the meat as compared to other methods of slaughtering.
4. Animal does not feel pain

The swift cutting of vessels of the neck disconnects the flow of blood to the nerve of the brain responsible for pain. Thus the animal does not feel pain. While dying, the animal struggles, writhers, shakes and kicks, not due to pain, but due to the contraction and relaxation of the muscles defecient in blood and due to the flow of blood out of the body...!!!

COASTAL CHAMA KUBWA....


Baada ya kusherekea Sikukuu ya Eid-el-Hajji hapo Jana
Mabingwa wa ligi daraja la kwanza (sasa ligi kuu) 1988,Coastal Union inshuka dimbani Kesho Jumapili ya terehe 28/10/2012 kukwaana Na JKT RUVU katika uwanja wa Azam Complex-Mbagala Dsm..

Ikiwa ni mechi yetu ya kumi(10) baada ya kufungwa mchezo mmoja tu na kutoa sare nne na kushinda michezo minne.Timu ya CUFC itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda 1-0 dhidi ya African Lyon na Kujikusanyia points 16.

CUFC inahitaji ushindi kesho ili kuwakikisha nia yetu kuwa Nafasi 3 za juu inatimia 
Huku ikiiombea dua mbaya leo Young Africans(Yanga) dhidi ya JKT Oljoro Kule Arusha na pia Azam na Simba-pale U/Taifa watoke angalau sare ili Pengo la Points lipungue .

Must Read and Maximum share on this Eid-ul-Azha...!!!

Thursday, October 25, 2012

Picha hii nimeipendaje...


Waandishi Tanzania wanaanza kujilinda wakiwa kazini...


Imam Khomein atoa salamu za Eid El Adh-haaaa...



Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mahujaji (2012/10/25 - 12:53)
 Hamdu zote ni za Allah, Mola Mlezi wa viumbe pia. Na rehema za Allah na salamu Zake zimfikie Mtume Mtukufu Mwaminifu na Aali zake watoharifu, wateule na masahaba wake wema. Msimu wa Hija uliojaa rehema na baraka umewadia na kwa mara nyingine na watu waliofanikiwa kwenda katika miadi hii iliyojaa nuru, wamo katika kumiminiwa baraka za Mwenyezi Mungu. Hapa, ninatoa mwito kwenu nyote mahujaji kutumia fursa ya kuwepo mahala hapa na kuwemo katika wakati huu, kujiimarisha kimaanawi na kimaada. Hapa, Waislamu wanaume kwa wanawake wanaitikia labeka mlingano wa Mola wao Mkubwa wa kujipamba kwa sifa na matendo mema; kwa nyoyo na midomo yao. Hapa watu wote wanapata fursa ya kufanya mazoezi ya kudumisha udugu, mshikamano na kujiepusha na maasi. Hii ni kambi ya malezi na mafunzo, ni maonyesho ya umoja, adhama na jinsi umma wa Uislamu ulivyokusanya pamoja sura za watu tofauti, ni kambi ya kupambana na shetani na mataghuti. Hapa Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima na Muweza amepafanya kuwa ni mahala ambapo waumini waweze kuona manufaa yao ndani yake. Tutakapofungua macho yetu ya busara na ibra basi ahadi ya mbinguni itaweza kuenea katika maisha yetu yote; ya kila mmoja wetu na ya jamii nzima. Sifa za kipekee za amali za Hija ni kule kuchanganya kwake dunia na Akhera na kuchanganya kwake masuala ya watu binafsi na ya kijamii. Al Kaaba isiyo na doa na iliyotukuka; kutufu miili na nyoyo za watu katika mhimili mmoja madhubuti na wa milele; amali ya Sai (baina ya Safa na Marwa) na kufanya jitihada za mfululizo na za mpangilio mmoja kutoka nukta ya kuanzia hadi nukta ya kuishia; kugura mahujaji wote kuelekea kwenye nyuga za ufufuo za Arafa na Mash'ar na shauku na uhudhurishaji wa moyo katika Mash'ar na maqam hayo adhimu, huleta unyofu na hali mpya, mapambano ya pamoja ya watu wote ya kukabiliana na vielelezo vya shetani, na hatimaye kwa pamoja na kutoka kila mahala na kila rangi na kila namna; wote wanashiriki kwa pamoja katika amali hizo tukufu zilizojaa neema na utukufu na zilizojaa maana na ishara za uongofu. Sifa za kipekee za faradhi hii zimejaa maana na madhumuni. Ni amali kama hii ndiyo ambayo inauunganisha moyo na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kuujaza nuru na kuunawirisha upweke wa moyo wa mwanadamu kwa imani na taqwa na wakati huo huo kumvua mwanadamu kutokana na mzingiro wa ubinafsi na kumsahilishia mambo katika jamii iliyopambika kwa sura za kila namna, ya umma wa Kiislamu na kumvisha nguo ya kujiepusha na madhambi ambayo huilinda roho yake kutokana na mashambulizi yaliyojaa sumu ya mashambulizi na vile vile humuongezea nguvu na moyo wa kupambana na mashetani na mataghuti. Ni mahala hapo ndipo ambapo hujaji anapoweza kuonana na Waislamu wenzake wengi wanaunda umma mkubwa wa Kiislamu na kuona kwa karibu nguvu na uwezo wa umma huo na hivyo kupata matumaini kuhusu mustakbali mwema na vile vile kupata hisia za wajibu wa kutoa mchango wake wa kuimarisha umma huo na pia kama atapata taufiki na msaada wa Mwenyezi Mungu aweze kutoa bay'a na kutangaza utiifu wake kwa Mtume (Muhammad) Mtukufu wa daraja na kufunga mithaki na ahadi imara kwa Uislamu azizi na kutia nia ya kweli ya kuijenga kiimani nafsi yake, kuleta marekebisho katika umma na kutia nguvu neno la Uislamu. Mambo yote haya mawili, yaani kuijenga nafsi na kuujenga umma (wa Kiislamu) ni faradhi zisizoishiwa na wakati na wala zisizofungwa. Njia za kuweza kufanikisha faradhi hizo mbili si nzito kwa watu wenye mazingatio na wanaoangalia mambo kwa kina katika utekelezaji wa majukumu ya kidini na kutumia vizuri akili, tabasuri na wenye mtazamo wa mbali. Kujenga nafsi huanzia kwenye kupambana na hisia za kishetani na kufanya juhudi za kujiepusha na madhambi na kujenga umma huingia sura kwa kumjua adui na njama zake, kufanya jitihada za kupelekea mashambulizi, hadaa na uadui wa maadui usiwe na athari zozote na hadi kufikia kwenye kuziunganisha nyoyo na mikono pamoja na lugha za matabaka yote ya Waislamu na mataifa yote ya Kiislamu. Katika wakati huu tulio nao hivi sasa, moja ya masuala muhimu zaidi ya umma wa Kiislamu ambalo lina mfungamano (wa moja kwa moja) na mustakbali wa umma wa Kiislamu, ni matukio ya mapinduzi katika nchi za kaskazini mwa Afrika na katika eneo la Mashariki ya Kati ambayo hadi sasa yameshapelekea kuanguka tawala kadhaa fasidi na vibaraka wa Marekani na waitifaki za Uzayuni na kuzitikisa tawala nyingine kama hizo. Kama Waislamu watapoteza fursa hii adhimu na iwapo watashindwa kutumia fursa hii katika kuujenga vizuri na kuleta marekebisho kwenye umma wa Kiislamu, basi watakuwa wamepata hasara kubwa. Hivi sasa mabeberu wavamizi na waingiliaji wa masuala ya ndani ya mataifa mengine wanafanya juhudi zao zote kujaribu kupotosha harakati hizo adhimu za Kiislamu. Katika harakati hizo kubwa, Waislamu wake kwa waume wamesimama kupambana na ukandamizaji wa watawala (wao madhalimu) na kupambana na udhibiti wa Marekani ambao umepelekea kudhalilishwa na kudunishwa mataifa ya Waislamu na kusababisha kushuhudiwa ushirikiano baina ya tawala za nchi hizo na utawala mtenda jinai wa Kizayuni. Waislamu wamegundua kuwa kitu kinachoweza kuwaokoa katika mapambano haya ya kufa na kupona ni Uislamu, mafundisho ya dini hiyo tukufu na nara na kaulimbiu zake zenye uwokovu na hilo wamelitangaza wazi wazi. Ajenda yao kuu wameifanya kuwa ni kulitetea taifa madhulumu la Palestina na kupambana na utawala ghasibu (wa Kizayuni). Wamenyoosha mkono wa urafiki kwa mataifa yote ya Waislamu na wanataka kuona umma wa Kiislamu unashikamana na kuwa kitu kimoja. Hii ndiyo misingi mikuu ya harakati za wananchi kwenye nchi ambazo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wananchi wake wamenyanyua bendera ya uhuru na mabadiliko na kujitokeza kwa viwiliwili na roho zao kwenye medani za mapinduzi na ni mambo kama haya ndiyo yanayoweza kuwa misingi mikuu ya kuleta marekebisho katika umma mkubwa wa Kiislamu. Kusimama imara na kushikamana vilivyo na misingi mikuu ni sharti la lazima la kuweza kupata ushindi wa mwisho wa harakati za wananchi kwenye nchi hizo. Lengo la adui ni kutaka kuhakikisha anateteresha misingi hii mikuu. Mikono fasidi ya Marekani na NATO na Uzayuni inatumia baadhi ya mighafala na mitazamo finyu kujaribu kupotosha wimbi la harakati ya vijana Waislamu na wanatumia jina la Uislamu kuwagombanisha Waislamu na wanaiita jihadi ya kupambana na ukoloni na Uzayuni kuwa ni ugaidi usio na macho katika ulimwengu wa Kiislamu ili Waislamu wauane wao kwa wao na hivyo maadui hao wa Uislamu waweze kuokoka na Uislamu na wanajihadi wake watazamwe kwa sura mbaya na chafu. Baada ya maadui kukata tamaa kwa kuona kuwa hawawezi kuushinda Uislamu wala kuzima nara na kaulimbiu zake, hivi sasa wameamua kuzusha fitna kati ya makundi tofauti ya Waislamu na wanafanya njama za kueneza chuki dhidi ya Ushia na chuki dhidi ya Usuni ili kuzuia kupatikana mshikamano na umoja katika umma wa Kiislamu. Maadui wanawatumia vibaraka wao katika eneo (la Mashariki ya Kati), kuzusha mgogoro nchini Syria ili kuzishughulisha akili za mataifa ya dunia na kuzifanya zisahau masuala muhimu ya nchi zao na zisahau pia hatari zinazowakabili. Maadui hao wanajaribu kuwashughulisha (Waislamu) na masuala ya umwagaji wa damu ambayo maadui wameyazusha wao wenyewe. Vita vya ndani nchini Syria na kuuliwa vijana wa Kiislamu kwa mikono ya Waislamu wenzao ni jinai ambazo zilianzishwa na Marekani na Uzayuni na tawala tiifu kwa maadui ambazo wanazidi kuchochea moto huo. Nani anaweza kuamini kuwa, tawala ambazo zilikuwa waungaji mkono wa madikteta waovu wa Misri na Tunisia na Libya, hivi sasa wamekuwa waungaji mkono wa kutaka demokrasia taifa la Syria? Kadhia ya Syria ni suala la kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa nchi hiyo ambao katika kipindi cha miongo mitatu ulikuwa umesimama peke yake kupambana na Wazayuni maghasibu na kuyaunga mkono makundi ya wanamuqawama wa Palestina na Lebanon. Sisi tunaliunga mkono taifa la Syria na tunapinga uchochezi na uingiliaji wa aina yoyote ile wa kigeni nchini humo. Marekebisho ya aina yoyote ile nchini humo inabidi yafanywe na wananchi wenyewe na kwa kutumia njia zinazokubaliwa kikamilifu na wananchi wa taifa hilo. Hatua ya mabeberu wa kimataifa ambao kwa msaada wa tawala za vibaraka wao katika eneo hili wanatumia kisingizio cha kuenea mgogoro na wakati huo huo kutumia kisingizio cha kuweko mgogoro kuhalalisha kufanya kila aina ya jinai nchini humo ni hatari kubwa ambayo kama tawala za eneo hili hazitajiepusha nayo basi inabidi zisubiri zamu yao ifike ya kukumbwa na hadaa hizo za kibeberu. Makaka na madada! Msimu wa Hija ni fursa ya kutaamali na kuyaangalia kwa kina masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu. Hatima ya mapinduzi ya eneo hili na juhudi za madola makubwa yaliyojeruhiwa kutokana na mapinduzi (ya wananchi wa eneo hili) za kutaka kuyapotosha mapinduzi hayo ni miongoni mwa masuala hayo (muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu ambayo inabidi kuyaangalia kwa kina). Njama za wasaliti za kutaka kuzusha hitilafu kati ya Waislamu na kuleta ugomvi na suutafahumu kati ya nchi ambazo zimeamua kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu; kadhia ya Palestina na juhudi za kuifanya itengwe na kuizima jihadi ya Wapalestina; propaganda za kueneza chuki dhidi ya Uislamu zinazofanywa na tawala za Magharibi na uungaji mkono wa tawala hizo kwa watu wanaomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW; kuandaa mazingira ya kuzuka vita vya ndani na kugawanywa vipande vipande baadhi ya nchi za Waislamu; kuzitisha tawala na wananchi wa nchi za Kiislamu zilizofanya mapinduzi kuhusiana na hatari za kupinga siasa za kibeberu za Magharibi na kueneza dhana potofu kuwa mustakbali wao unategemea kujisalimisha kwao mbele na madola ya kibeberu na masuala mengine muhimu sana kama hayo, ni miongoni mwa kadhia muhimu ambazo inabidi ziangaliwe kwa taamuli na kwa mazingatio makubwa katika fursa inayopatikana kwenye Hija na chini ya kivuli ya kupendana na kuwa na fikra moja nyinyi mahujaji. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Sayyid Ali Khamenei, 30/Mehr/1391 (Hijria Shamsia) inayosadifiana na tarehe tano Dhulhijjah 1433 Hijria.

Ndugai atoa ufafanuzikuhusu ripoti ya bunge...


Na Rodrick Minja,Dodoma
RIPOTI ya bunge kuhusu tuhuma za wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa,inatarajia kuwasilishwa bunge wiki lijalo. Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Spika wa bunge Anne Makinda atatoa utaratibu wa namna ya kuwasilisha ripoti hiyo ndani ya ukumbi wa bunge. Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa kwa mujibu wa Kanuni za bunge toleop la 2007, vifungu 114(17), na 119 (1) hadi (6) kwa pamoja vinampa madaraka spika kuhusu utaratibu wa kufuata katika uwasilishaji wa taarifa bungeni. “Ambapo, yaweza kuwa spika akatoa uamuzi ama kamati kuwasilisha taarifa hiyo bungeni au vinginevyo lakini spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi huo bungeni wakati wa mkutano wa tisa wa bunge unaotarajia kuanza oktoba 30 mwaka huu,” alisema Ndugai. Katika mkutano wa nane wa bunge lililopita, Spika wa bunge Anne Makinda aliunda kamati ya kuchunguza tuhuma za wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini kuhusu kujihusisha na vitendo vya rushwa. Makinda alifia uamuzi huo kufuatia tuhuma zilizokuw zimezagaa karibu nchi nzima kuwa wabunge hao wamekuwa wakijihusisha na rushwa lakini wakiwa bungeni Mbunge wa Nkasi Ali Keissy Mohamed ndiye aliyeanzisha chokonoko hizo kabla ya wabunge wengine kuidandia ajenda hiyo. Kamati iliyoundwa na spika ilikuwa chini ya Mbunge wa Mlalo Hassan Ngwilizi ambaye alisaidiwa na wajumbe Said Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki),Godbless Blandes (Karagwe) pamoja na Mbunge wea Viti Maalumu Ridhiki Juma. Kwa mujibu wa Ndugai, Kamati hiyo ilimaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa spika tangu Septemba 20 mwaka huu ambapo ndiyo siku ilipokabidhiwa kwa spika. Kwa upande mwingine Naibu spika alikemea vitendo vya baadhi ya watu na vyombo vya habari kuendelea kuanaidka na kuchapisha juu ya kilichomo ndani ya ripoti hiyo kwa maelezo kuwa ni kosa. “Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyokatika vyombo vya habari ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge kw mujibu w kifungu cha 31 (1) (g) cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya bunge sura 296,” alisisitiza Ndugai. Alifafanua kuwa kifungu hicho kinakata mtu yeyote kuchambua taarifa ya kamati kabla ya taarifa hiyo kuwasilishwa bungeni. Naibu Spika alieleza kuwa ikibainika kuwa taarifa imechapishwa wahusika wanaweza kulipa faini isiyozidi Sh 500,0000 au kifungu kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Chanzo: Mjengwa blog

Sasa wanaanza kuandamwa viongozi wa BAKWATA...



Picha ya juu na chini zinaonyesha namna jeshi la polisi lilivyoshughulika kufuatia kupigwa kitu kinachohisiwa ni bomu nyumbani kwa katibu wa bakwata mkoa wa Arusha Abdul Kareem Jonjo.

Baadhi ya vongozi wa ulinzi na usalama mkoani humo wakiongozwa na mkuu wa mkoa walikuwa kwenye matukio mbali mbali nyumbani na hospitalini jijini humo mtaa wa kanisani kata ya Sokoni.
(picha na zote na mahmoud Ahmad)

Serikali yajipanga....

 Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakipitia Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini   wakati wa  kikao hicho cha kazi (retreat)  cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali  kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika  ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.


Viongozi hawa wakichangia katika kikao hicho cha siku tatu kinachofanyika mjini Dodoma...

Mawakili wa Uamsho wajitoa kuwatetea wanauamsho kutokana na usumbufu wanaofanyiwa na mahakama.


 Huyu ni Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita waliopelekwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi na kuhatarisha amani katika nchi.

                                                     Mahakama Kuu ya Zanzibar.
  
Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma na Salim Tawfik walizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na usumbufu wanaofanyiwa wateja wao  kuhangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafaka.



Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Msiba hauna kadi wala mwaliko....

                   Nilipofika Korogwe nilianzia Masuguru kuangalia Ngombe wa babu Katani..




 Hizo picha za juu watu hawaziki,bali ni vijana wanaandaa kaburi. nami nilishiriki kuandaa kaburi la dada Mwanasha. Nilifurahishwa sana na maisha ya wakazi wa Korogwe, hakuna kuwalipa wachimba makaburi. Mtu akipatwa na msiba vijana wote katika kijiji wanapigiwa mbiu na kuelekea makaburini kuchimba kaburi, wanachopewa ni ndoo ya maji, uji ama chai. safi sana, Mjini huku kaburi maka uwe na laki moja au zaidi.

 Hapanilikuwa naandaa jeneza la dada, naam waislam hatuagi maiti. Ila kuna kitu kinaitwa kupamba jeneza, unalifunika jeneza kwa shuka na vitambaa, kama ni la mwanamke linawekwa khanga, kama ni la mwanaume linawekwa shuka tupu. Nilijifunza juzi mambo hayo. Ndiyo raha ya kukaa karibu na wazee.

 Huyo mnene kabisa ni mdogo wetu sote wawili hapo. Anaitwa Mustapha, mtoto wa mama mkubwa, baba yake ndie aliekuwa mmiliki wa ile hoteli maarufu Korogwe ya 'River Side' kwa waliopita Korogwe lazima wanaijua Hoteli ile maana ipo barabarani kabisa karibu na gereza la korogwe.

 Mapacha watatu, wa kwanza kutoka kushoto ni mtoto wa mama mkubwa anaitwa Hussein Ally, wa pili ni dogo langu Juma Kido na wa tatu ni jembe mwenyewe, baada ya mazishi tukaamua kujipumzisha kidogo. Korogwe pamekuwa pazuri jamani.

Tatizo la mdogo wangu huyu Juma Kido, akipata upenyo kidogo anauchapa usingizi..........


Ndugu zangu,

Ukisikia mtu anasema maiti ya mwenzio gogo wala usimlaumu. Maana juzi nilipata msiba wa dada bila ya kutegemea. Nikiwa katika mizunguko yangu kaka mtoto wa shangazi akanipigia simu kuniuliza nyumbani kijitonyama kuna nini?

Nikawa sijui kitu, nikampigia mdogo wangu wa kike Nafisa Kido, huku analia akanambia dada Mwanasha ameletwa nyumbani akiwa maiti. Awali sikumuelewa,na kichwani nikawa nimechanganyikiwa. Nilichofanya ni kukatisha mizunguko yangu na kurudi nyumbani.

Nilipofika nikamkuta mjomba Selemani Katani (baba mmoja na mama yangu mzazi Rehema Katani). Akiwa nyumbani amejiinamia macho yamemuiva kwa kulia; naam ukimuona mtu mzima analia ujue kuna jambo.

Nikapatwa na dukuduku rohoni, machozi ya mwanaume yapo mbali sana hasa baada ya kugundua mimi ndie kaka pekee pale nyumbani. Nyumba nzima wanaume tulikuwa mimi na mjomba. Hivyo kulia ni udhaifu.

Mwanasha Selemeni Juma Katani, ni mtoto wa mjomba, alikuwa ni mdogo kwangu kwa miaka zaidi ya mitano. Lakini kwa kuwa ni mwanamke anakuwa mkubwa, maana tayari alishazaa watoto wanne, wa mwisho ni mdogo ana miezi chini ya sita. Na ndie aliesababisha kifo chake.

 Ndivyo, hakutakiwa kubeba ujauzito kwa mujibu wa daktari, lakini kwa bahati mbaya ama nzuri akapata ujauzito mwingine kutoka kwa mumewe wa halali kabisa. Alijifungua kwa taabu sana tena baada ya kuwahishwa na gari ya wagonjwa kutoka Hospitali ya Korogwe- Magunga kuenda Bombo Tanga mjini.

Tangu siku hiyo alisumbuliwa na moyo mkubwa, mauti yalimkuta ndani ya gari akipelekwa Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam kupata matibabu. Alitoka Korogwe siku ya jumanne, nadhani mitikisiko ya safari ilisababisha mauti yake.

Wakati anashushwa kutoka ndani ya Basi la Burudani ili apakiwe katika Tax kuelekea Hospitali moja kwa moja. Ndipo roho ikaacha mwili, ikabidi safari ya hospitali iahirishwe maiti apelekwe nyumbani Kijitonyama alimaua.

Baada ya hapo kilichofuata ni kusafirisha maiti kwa ajili ya maziko mjini Korogwe eneo la Masuguru. Mungu ailaze roho ya marehemu.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
25/10/2012  


Monday, October 22, 2012

What I learnt from the Muslim riots in Zanzibar and the mainland ...


 NB: For any grammatical errors blame my nursery school English teacher...


First allow me to declare interest in Islam. For I am a Muslim and clean one. So in this article, if I slipped and defending Islam in a way that will build the questions please forgive me readers, it is not my fault.

Two weeks ago there was a two events concerned Muslims as if they were planned, one took place in Dar es Salaam Mbagala areas for 14 years young profaning the Quran. The second incident occurred in Zanzibar after the Revival leader Sheikh Farid allegedly lost under controversial circumstances.

These two events when tested seriously were not supposed to happen if our government treat them seriously by using wisdom and experience, something that even the Muslim community had failed to do.

Limitations of wisdom defect are the cause of all violence in Zanzibar and the mainland. Also foreign countries, especially the Arabic financing the incidents occurs in a large percentage that is another source. And this is according to my thinking and not anyone I've heard. But it is how the events happened.

Let's start with Shaikh Issa Ponda, he is secretary of the Muslim communities and institutions in Tanzania. He was arrested on charges of fueling violence and breach of the peace in the country.

The main reason for violence Mbagala off a deadly three churches burned and badly damaged after the young man's urinary book Quran as a controversy of a child and another who claimed he was a Muslim. He told Christian young man that anyone urinary holy book will turn mouse or other information says he will turn the snake.

Another reason for the arrest of Sheikh Ponda is the invasion of compound numbers 311/3/4 Chang'ombe located near the national stadium assets of the Agritanza Company.

The young boy was already in police custody. Legal the boy were a criminal, because according to our constitution one should not ignore the other religions because everyone has the freedom and the boundaries of worship, although the government has no religion. Group of people to give up a criminal in a police station is a legal offense even in Mecca and Medina, where Islam started this action would not be accepted.

Point of correction I don’t mean the act of abusing Quran, but the act of invading the police station and demanded the criminal so that you can panish them on your way it is not tolerated. And every Muslim in Tanzania knows that.

The second mistake is that in every demonstrations or violence, Muslims and non-Muslims, thieves and civilized, sane and mad are getting involved by default or deliberately. So it is quite possible that the one who destroys the churches not only Muslims but criminals who have used the back of a demonstration greenhouse fulfill their mission.

The teachings of Islam does not accept theft (something that happened in that rally).  Do not accept doctrine of environmental damage in the war (something that happened), here I will explain.

Islam teaches (accept) war against non-Muslims if they assaulted them out of their homes. But in war God and His Messenger have said the Muslim should not cut down trees, burning houses of worship. (And this even Basaleh Sheikh of the mosque's imam, who have not heard Fugitive those involved violence, served They spoke that Islam respects houses of worship and should not be damaged, especially if they have not been destroyed to you). Now this knowledge to burn churches where you get from?

The second mistake in the desecration of God's Book of Truth (the Quran), I heard no single leader of the church to provide a declaration of contempt or hypocritical act against that. Now burning the churches is the respond to young man who was influenced by the other young Muslim or Christian as a whole?

Another thing the boy was influenced by another boy who took the holly Quran from home and ordered his friend to do what he did and there is information that they bet he will turn animal, but where is this muslim boy if I may ask?

Here I beg to be understood, not even a little hypocritical act that, even that thing could be done by an infant who know nothing about faith and religion, I could stand on the side of Islam and not otherwise. But the kind of respond and actions taken due to the act is what put me into dilemma.

On the second occasion to attack the compound the fault is on BAKWATA, Muslim Council of Tanzania who are legally recognized by the government. They sold the plot what is legal was Waqfu (Waqfu, is any property that is an inheritance for Muslims of the area or country. Were some rich Muslims who do not have relatives died, they decided to give their property to Muslims, it is waqfu).

If  BAKWATA are the one who sold the plot that is legal agreements, not be a scholar and an understanding of things like Sheikh Ponda doing things.

Such violence was supposed to happen at BAKWATA area for the property has already been of the buyer; attack is the interference with freedom of man. He can call you a thief and a robber and the court find you guilt no any lawyer could win that case.

Because the buyer already had all the documents and contracts to possess property laws and regulations that the plot is already his. Attack is aggression and lack of insight.

The third mistake is when Sheikh Ponda was arrested and then the Muslims began pressuring the government to let him free. It is nonsense to interfere with the independence of the judiciary. And this is the new maneuvers of the Government of Tanzania. Whenever they find that thay have slipped a place quickly ran to the court, so basically Muslims were too late to ask the government release him. For even the government has no power because courts are independent.

The fourth mistake made by Muslims is when they fail to use the only chance they had to surprise the government and its agencies including the police force.

Commander Suleiman Kova, head of the special police in Dar es Salaam region, declared last Wednesday that anyone who thinks to Sheikh Ponda then should surrender as quickly as possible to the police. All mosques in Dar es Salaam announced after Friday prayers that they are going to surrender to Kova.

But out of nothing the very friday morning things turned upside down and the move were to the State house to meet the president, while many were absent in the president knew he was on tour in Oman.

Here is where the controversial starts, why did they change their minds because they felt if they were going to surrender the government will just lead their way without tear gas or nothing. And here is where I believe Muslims in Tanzania are being used by people who are outside the country for their own interests. Their expectation is to see people killed by police or hurt them is the way to portray the community that they are often oppressed.

If I were the Muslim adviser I would asked them to stand their ground to go for Kova by using non violence tactic. Tanzania has many Muslims, if we all decide we're going to  Commander Kova peacefully and without violence. Do you think what the impact we could make? Both wear their white coats while they mention the name of Allah and His Messenger stable without violence. What about that?

When they (Polise) ask them what they want, the role we are followers of Sheikh Ponda we've come to surrender we would be sent to court. Only a small number of Muslims in Tanzania who will support this idea for instance ten million Muslims, I do not think the government will serve ten million inmates while they continue to listen to their case. Sheikh Ponda must have been released even by twisting the law.

Leave that alone, lets shift to Zanzibar, revival sheikh has his thing. For I do not agree with the fact that he was abducted for this episode is too miraculously wise people have begun to identify some strategic mistakes made by the group's members who were appointed by false revival.

It is impossible for a person to be interrogated by security officer under the suspect of destroying the country then return back as fresh as from his mothers’ womb. I do not mean security guys are cruel but it is just that the kind of person is too radical to them.

Sheikh said that the day of the event he pulled up the phone and someone introduced as his disciple, was not known nor ever met him. For the Sheikh's at this situation to go and meet someone he don’t even know then without any security, leave me with a lot of questions and generate suspicious that it is planed.

And even the details of his abduction is not clear and coherently to understand. For he says he arrived in the area around the mosque at Mbweni area, saying his sent his driver to buy electronics, with him went to the mosque for a short call.

That is very unusual allows your nearest person to leave the area in which you are going to meet someone who you don’t know, again buying electricity is not an emergency you can even buy it on your way home.

Then the second scenario is that just few hours when the information about the disappearance of Sheikh  spread violence started immediately burn and destroy the dwelling of CCM. Why CCM?

CCM is a party like the other parties in Zanzibar, CCM is not the government, as their anger against the government were, why they did not set fire to and destroyed the homes of members of the CUF? For Zanzibar now dominated by two parties where CCM and CUF called government of national unity.

Why wouldn’t they make the patient even though after two or three days and then they began to show their anger? The answer is simple, they had already Revival of abduction fear their leader any day, so why do their Sheikh precaution was not taken early?

Here is what was requested to be done, and even violent abduction meant to also warrant by the sheikh's why he returned home without any dent. Do not play with the government, they would not agree to hold a person for four days and then let him go just like that with all secrets of the questions he posed to.

If they want to put it that way, they don’t have to blame the government of Zanzibar they should read the history of the cruelty of the first president of that land whoever had been arrested his relative what they find is his dead body or you have a permanent defect.
Allow me to end up here today, but my head has so many things that I have learned from talking to these two weeks of violence.

For example, there are Muslims who wanted to blame Mr president by marching to the palace because he had sent condolence to Christians and go to visit churches damaged in Mbagala.

I do not know if the Muslims knew what they were demanding, the police force is under the president, who is also a Muslim. Ispector General of Police (IGP) Said Mwema is also a Muslim, Regional Police Commander (RPC) Suleiman Kova is also Muslim, dint they see all that and bend the law to fever you?

Already the boy were in Police hands, why did not give them time to make decisions but decided to demonstrate to the police station?

What kind of president will Kikwete be if he stand in public that he is the leader's blessing upon crime and violated the laws of the land? I do not want to believe if any Muslims were expected after they disturb the peace and destroy wealth, President Kikwete would stand up and say 'okay okay you did a very good job these Muslims destroy Christian churches are very savages'. I do not know maybe my mind does not know the figure, but if Kikwete was speaking these words .....

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/0752 593894
kidojembe@yahoo.com
22/10/2012

Nilichojifunza vurugu za Waislamu Tanzania bara na visiwani....




Kwanza naomba ‘ku-declare interest’ kwa Kiswahili wanasema kukubali kuwa na maslahi katika Uislamu. Maana nami ni muislamu tena safi. Hivyo katika makala haya ikiwa nitateleza na kuutetea Uislamu katika namna ambayo itakujengea maswali naomba mnisamehe wasomaji, si kupenda kwangu.

Wiki mbili zilizopita kulitokea matukio mawili yaliyoongozana utadhani yalipangwa, moja lilitokea mjini Dar es Salaam maeneo ya Mbagala kwa kijana wa miaka 14 kuinajisi Quran. Tukio la pili lilitokea mjini Zanzibar baada ya kiongozi wa Uamsho Sheikh Farid kudaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Matukio haya mawili ukiyapima kwa umakini hayakupasa kutokea ikiwa Serikali yetu ingeyachukulia kwa uzito wake na kuyaamua kwa kutumia hekima kitu ambacho hata jamii ya waislamu walishindwa kukifanya.

Upungufu wa hekima ndicho kilema kilichosababisha machafuko yote Zanzibar na Bara. Pia kutumika kisiasa na mataifa ya nje hasa ya kiarabu limeonekana kwa asilimia kubwa kuwa ni chanzo kingine. Na hili ni kwa mujibu wangu wala sijasikia kwa mtu yeyote. Bali ni namna matukio yalivyotokea.

Tuanze na sheikh Ponda Issa Ponda, huyu ni katibu wa jumuiya na taasisi za Kiislamu Tanzania. Yeye alikamatwa kwa tuhuma za kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini.

Sababu kuu mbali ya vurugu za mbagala zilizosababisha makanisa matatu kuchomwa na kuharibiwa vibaya baada ya kijana mmoja kukojolea kitabu cha Quran ikiwa ni ubishani wa kitoto na mwenzie ambae inadaiwa alikuwa muislamu. Alimwambia kijana huyo wa kikristo kuwa mtu yeyote akikojolea kitabu hicho kitukufu atageuka panya au maelezo mengine yanasema atageuka nyoka.

Sababu nyingine ya kukamatwa kwa Sheikh Ponda ni uvamizi wa kiwanja namba 311/3/4 kilichopo Chang’ombe karibu na uwanja wa taifa mali ya kampuni ya Agritanza.

Nilitangulia kusema hekima ingetumika balaa hili lisingetokea ni kuwa mtoto yule (alieidharau Quran) tayari alikuwa mikononi mwa polisi. Kisheria ni mhalifu, maana kwa mujibu wa katiba yetu mtu hatakiwi kudharau dini ya mwenzie kwasababu kila mtu anao uhuru na mipaka ya kuabudu ingawa serikali haina dini. Kundi la watu kuenda kumtoa mhalifu katika kituo cha polisi ni kosa kisheria hata huko Makka na Madina dini ya kiislamu ilipoanza tendo hili lisingeweza kukubalika.

Simaanishi tendo la kunajisi Quran, bali kitendo cha wananchi kuvamia kituo cha polisi na kutaka kumtoa mhalifu mkamuhukumu mnavyojua nyinyi.

Kitu cha pili maandamano ama vurugu zinavutia watu wengi, waislamu na wasio waislamu. Wezi na wastaarabu, wenye akili timamu na wendawazimu. Hivyo inawezekana kabisa walioharibu makanisa  si waislamu bali ni wahuni tu ambao wametumia mgongo wa maandamano kutimiza dhamira zao chafu.

Mafundisho ya dini ya kiislamu hayakubali wizi (kitu ambacho kilifanyika). Mafundisho hayakubali uharibufu wa mazingira katika vita (kitu ambacho kilifanyika) hapa nitafafanua.

Dini ya kiislamu imefaradhisha (kukubali) vita na wasio waislamu ikiwa watawanyanyasa na kuwatoa katika majumba yao. Lakini katika vita hivyo Mungu na Mtume wake wamesema haitakiwi kwa Muislamu kukata miti, kuchoma nyumba za ibada. (Tena hili hata Sheikh Basaleh imamu wa msikiti wa Mtoro ambae sikumsikia kushiriki vurugu zile, aliwahi kulizungumza kuwa Uislamu unaheshimu nyumba za ibada na haifai kuharibiwa hasa ikiwa wao hawajaharibu za kwenu). Sasa elimu hii ya kuchoma makanisa imetoka wapi?

Kitu cha pili katika kunajisiwa kitabu cha Mungu wa kweli (Quran), sikusikia kiongozi hata mmoja wa kanisa kutoa tamko la kudharau ama kuafiki kitendo kile. Sasa kuchoma makanisa ni kudhihirisha hasira kwa yule kijana mdogo ambae alishawishiwa na kijana mwenzie wa kiislamu ama ni hasira kwa ukristo?

Kitu kingine yule kijana alietoka na msahafu nyumbani kwao na kumuamuru rafiki yake aukojolee ambapo atageuka mnyama yeye yupo wapi? Maana kama ni makosa wametenda pamoja kutokana na utoto wao.

Hapa naomba nieleweke, siafiki hata kidogo kitendo kile, hata kingefanywa na motto mchanga basi ningekuwa upande wa wailsamu na si vinginevyo. Ila hatua zilizochukuliwa kutokana na kitendo kile ndizo zinazonitatiza.

Kuhusu tukio la pili la kuvamia kiwanja makosa ni ya BAKWATA, baraza la Waislamu Tanzania ambao kisheria wanatambulika na Serikali. Wao waliuza kiwanja kile ambacho kisheria kilikuwa Waqfu (Waqfu, ni mali yoyote ambayo inawachwa kuwa urithi kwa waislamu wa eneo ama nchi. Wapo Waislamu matajiri ambao wanakufa hawana ndugu, wanaamua mali zao wanazitoa kwa waislamu, hiyo ndiyo waqfu).

Ikiwa bakwata ndiwo waliouza kiwanja kile na mikataba ilishawekwa kisheria, haikutakiwa mtu msomi na mwenye uelewa wa mambo kama Sheikh Ponda kutenda mambo yale.

Ilitakiwa vurugu hizo akazifanyie bakwata ambae ndie alieuza, kwa maana tayari mali ile imeshakuwa ya mnunuaji, kumvamia ni kuingilia uhuru wa mtu. Anaweza kukuita jambazi ama mwizi na mahakama ikakuhukumu bila mwanasheria yoyote aliekubuhu kuweza kushinda kesi hiyo.

Kwasababu mnunuzji tayari alikuwa na hati na mikataba yote ya kuimiliki mali ile kisheria na kitaratibu tayari ni yak wake. Kumvamia ni uchokozi na kukosa busara.

Kosa la tatu ni pale Sheikh Ponda alipokamatwa halafu waislamu wakaanza kuishinikiza Serikali kumwachia kinguvu. Ni upuuzi kuingilia uhuru wa mahakama. Na huu ni ujanja mpya wa Serikali ya Tanzania. Wanapogundua wameteleza mahala haraka wanakimbilia mahakamani, hivyo kimsingi waislamu walishachelewa kuitaka serikali kumuachia sheikh wao, maana mtu amabe ameshasimama mahakamani hawezi kutolewa tena. Maana hata hiyo serikali haina uwezo kwani mahakama ni mhimili wa dola unaojitegemea.

Kosa la nne lililofanywa na waislamu ni pale waliposhindwa kuitumia nafasi pekee waliyokuwa nayo kuiduwaza serikali na vyombo vyake likiwemo jeshi la polisi.

Kamanda Suleiman Kova, mkuu wa jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam, alitamka siku ya jumatano iliyopita kuwa mtu yeyote ambae anaona yupo chini ya Sheikh Ponda basi ajisalimishe haraka kwa jeshi la polisi. Misikiti yote jijini Dar es Salaam ilitangaza baada ya sala ya ijumaa kuwa watakwenda kujisalimisha kwa Kova.

Lakini cha ajabu asubuhi ya siku hiyo mambo yakabadilishwa na kusema wanakwenda ikulu kuonana na rais ilhali wengi walikuwa wakijua rais hayupo nchini alikuwa ziarani nchini Oman.Maana waliona wakienda kujisalimisha serikali haitawaandama kwa mabomu kwani mtu anaejisalimisha hatakiwi kupigwa. Na hapa ndipo ninapoamini waislamu wa Tanzania wanatumiwa na watu walio nje ya nchi kwa maslahi yao. Kwani watu wakiuwawa na jeshi la polisi ama kuumizwa kwao hiona ndiyo njia sahihi ya kuionyesha jamii kuwa wanaonewa.

Ningekuwa mshauri wa waislamu nchini ningewataka kusimamia msimamo wao uleule wa kuenda kujislaimisha kwa Kova. Jiulize Tanzania ina waislamu wangapi, sote tuamue Tanzania nzima tunakwenda kujisalimisha kwa kamanda Kova kwa amani bila vurugu. Unadhani Dar es Salaam itakalika? Wote wavae kanzu zao nyeupe huku wanataja jina la Mungu na Mtume wake kiutulivu bila ghasia. Hilo vipi?

Wakiulizwa mnataka nini, wajibu sisi ni wafuasi wa sheikh Ponda tumekuja kujisalimisha tunataka kupelekwa mahakamani. Nikitaja idadi ndogo tu ya waislamu Tanzania ambao wataunga mkono wazo hilo mathalan waislamu milioni kumi wajisalimishe, sidhani serikali itaweza kuwahudumia mahabusu milioni kumi wakati wakiendelea kusikiliza kesi yao. Lazima Sheikh Ponda angeachiwa huru tu hata kwa kupindisha sheria.

Tukiachana na hapa bara tuhamie Zanzibar, sheikh wa uamsho ana lake jambo. Maana sikubaliani na ukweli kuwa alitekwa maana jambo hili limefanyika kimaajabu sana hata wenye akili wameshaanza kubaini baadhi ya makosa ya kimkakati yaliyofanywa na kikundi hicho cha wanauamsho kwa uongo walioufanya kuwa ni kweli.

Haiwezekani mtu aliekamatwa kwa ajili ya mahojiano mazito kama hayo ya kuhujumu nchi halafu asirudi na alama hata ya kufinywa. Mimi si mwana usalama lakini wanausalama nawajua, hasa wanapokuwa na mtu mkaidi kama Sheikh Farid.

Sheikh huyo anasema siku ya tukio alipigiwa simu na mtu aliejitambulisha ni mwanafunzi wake, hakuwa akimjua wala kuwahi kuonanan na huyo mtu aliempigia simu. Kwa Sheikh wa kikundi kama uamsho kuenda sehemu aliyoitwa na mtu asiemfahamu tena bila ulinzi kwa kipindi hiki ambacho Tanzania alishatekwa kiongozi wa madaktari na kuteswa vibaya si jambo la kuingia akilini.

Na hata maelezo ya kutekwa kwake hayaingii akilini kwabisa. Maana anasema alipofika katika eneo la Mbweni karibu na msikitimdogousiotumika na watu wengi aliamua kushuka na kumwamuru dereva wake akanunue umeme, nae alikwenda msikitini kwa ajili ya haja ndogo.

Yaani ni kitu cha ajabu sana unamruhusu mtu wako wa karibu kuondoka eneo ambalo unakwenda kukutana na mtu ambae humjui, tena kwa dharura ndogo kama ya kununua umeme kitu ambacho ungekifanya hata wakati unarudi nyumbani.

Halafu kitu cha pili taarifa za kupotea Sheikh huyo zilisambaa haraka zikiambatana na vurugu za kuchoma na kuharibu maskani za CCM. Kwanini CCM?

CCM ni chama tu kama vyama vingine, CCM si serikali, kama hasira zao zilikuwa ni dhidi ya serikali kwanini hawakuchoma moto na kuharibu majumba ya chama cha wananchi CUF? Maana Zanzibar sasa inaongozwa na vyama viwili CCM na CUF ambapo inaitwa Serikali ya umoja wa kitaifa.

Halafu kupotea kwake kwanini kunasibishwe na kutekwa? Kwanini wasingefanya subira japo baada ya siku mbili ama tatu ndipo wakaanza kuonyesha hasira zao? Jibu ni rahisi, tayari wanauamsho walishakuwa na hofu ya kutekwa kiongozi wao siku yoyote, sasa kwanini Sheikh wao huyo hakuchukua hadhari mapema?

Hapa pana kitu kilitakiwa kifanyike, vurugu zilipangwa na hata kutekwa kwa sheikh huyo pia kulipangwa na ndiyo maana amerudi nyumbani bila mchubuko. Usifanye mchezo na chombo cha dola, wasingekubali kumshikilia mtu kwa siku nne halafu wamuachie akatoe siri za maswali aliyoulizwa.

Kamakweli wanataka kuitia ila serikali ya Dk Shein rais wa Zanzibar basi wasome historia za ukatili wa rais wa kwanza wan chi hiyo ambae alikuwa akimkamata mtu kinachopatikana ni mwili wake tena ukiwa mfu ama una kilema cha kudumu.
Naomba leo niishie hapa, lakini kichwa changu kina mambo mengi sana ya kuzungumza ambayo nimejifunza kutokana na wiki mbili hizi za vurugu. Waislam tumeingia do asana kwa kuonekana ni wakorofi na hatuna simile.

Mathalan, wapo waislamu amabao walitaka kuandamana mpaka ikulu ili kumsemarais kwanini amewapa pole wakristo na kuenda kutembelea makanisa yaliyoharibiwa huko mbagala.

Sijui kama hao waislamu wanajua walichokuwa wakikidai, jeshi la polisi lipo chini ya rais ambae ni muislamu pia. Tayari kijana alieidharau Quran alishafika mikononi mwake rais, hamkumpa muda afanye maamuzi mkaandamana mpaka kituo cha polisi kutaka kumpora kijana huyo ili mumuadhibu mnavyojua nyinyi, matokeo yake badala ya kutoa adhabu kwa muhalifu mkaamua kufanya uhalifu kwa kuharibu mali.

Ni rais wa aina gani atakaesimama mbele ya umma ambao yeye ni kiongozi abariki uhalifu na kukiukwa sheria za nchi? Sitaki kuamini kama wapo waislamu walitegemea baada ya wao kuvuruga amani na kuharibu mali asubuhi yake rais Kikwete angesimama na kusema ‘sawa sawa mmefanya kazi nzuri sana waislamu kwa kuharibu makanisa hawa wakristo ni washenzi sana’. Sijui labda akili yangu haijui kufikiri lakini laiti Kikwete angezungumza maneno hayo…..

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894   
22/10/2012

      

Viongozi wa Kenya ziarani Tanzania...

 Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya
wakati walipomtembelea ikulu ya Tanznia jana.

 Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na  Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya, ambae pia anawania urais nchini humo.


Mbali ya Uhuru Kenyata na Wamalwa Rais Kikwete, katika mazungumzo hayo pia alikutana na  
Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012

PICHA NA IKULU
<

Kikwete afunga rasmi uchaguzi wa umoja wa wanawake wa Tanzania.

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).


 Hapa akizungumza chochote kabla hajafunga mkutano huo uliomrudisha madarakani mwenyekiti wa UWT bi Sofia Simba, waziri wa wanawake jinsia na watoto.

                 Kikwete akisalimiana na wakongwe wa UWT 

Saturday, October 20, 2012

Dada huyooo ameolewaa.... mahaariii ishatolewaa...

Aunt Ezekiel, mwigizaji maarufu kwa kuvaa viguo vya uchokozi akisaini cheti cha ndoa ikidhihirisha amekuwa Muislam. Baada ya kufunga ndoa na tayari yupo katika mchakato wa kuelekea uarabuni kujiunga na mumewe siku yoyote kuanzia leo.

kidojembe iliwahi kuripoti juu ya sakata la dada huyu kuiomba jamii ya watanzania radhi kufuatia kuonyesha utupu katika tamasha la muziki la fiesta mjini Dodoma. Na katika maombi hayo alisema anaweza kuolewa siku za karibuni hivyo wakwe zake pia watafurahi ikiwa watanzania watamsamehe. Kumbe alikuwa hasemi uongo, ameolewa kweli....

Hivi watu kama hawa wanajua kama Waislam wameandamana?


Karibu mzee,lakini nchini waislam wamechachamaa wanataka haki yao.....

Makamu wa Rais Dk Bilal akimkaribisha nchini Rais Jakaya Kikwete jana baada ya kuwa nchini Oman kwa siku kadhaa katika ziara ya kikazi. Na kwa bahati mbaya kwa siku tatu mfululizo tangu Rais akiwa nje ya nchi Dar es Salaam ilikuwa ikiwaka moto kwa vurugu baada ya Sheikh Ponda Issa Ponda kukamatwa.

Taarifa zilizotufikia hivi punde.....


 Kikundi cha UAMSHO mjini Zanzibar kimesema Kiongozi huyo amepatikana hai usiku wa kuamkia leo. kabla uamsho waliipa serikali masaa 26 hadi leo alasiri amiri wao awe amepatikana vinginevyo hali itakuwa mbaya.

UAMSHO ni kikundi cha kiislam kinachodai haki ya kujitenga kwa Tanganyika na Zanzibar kwa madai muungano unawaharibia utamaduni wao. Wiki iliyopita kiongozi huyo Sheikh Farid Ahmed (pichani) aliripotiwa kutekwa nyara na watu wa usalama wa taifa hivyo kufanya kutokea vurugu kwabwa baina ya serikali na waislam mjini humo.

Vurugu hizo zilizosababisha kifo cha askari mmoja wa FFU, CPL Said Abdulrahman pamoja na mwananchi mmoja Salum Muhoja.  

Wanajeshi walikuwa wanatoka Lugalo wanakwenda kutuliza ghasia mjini.... Fuata kilichotokea maeneo ya Tabata.....

                                               Kwanza waliwekwa sana kwenye foleni....

 Uzalendo ulipowashinda wakaamua kumtafuta trafik aliehusika kuwaweka sana kwenye foleni ya magari.

 Wananchi wakaanza kuvutiwa na picha hiyo ya bure wakakusanyika kuona kitakachofuata.

Ilibidi hekima itumike kumaliza ubishi huo, maana badala ya FFU kutuliza vurugu za Waislam wangekuja kutuliza vurugu za trafik na wanajeshi.


Wanajeshi wanaokadiriwa kuwa 50 kwa pamoja wamemshambulia trafiki kwenye taa za ubungo na kuondoka kwa madai kuwa kawachelewesha kwenye foleni, baada ya kuondoka magari hayo ya jeshi yalizuiwa kwa muda wa zaidi ya saa moja maeneo ya Tabata dampo. kabla ya kuachiwa kuendelea na safari yake.

Picha na Mjengwablog