Tuesday, October 2, 2012

Jembe jana nilikutana na ndugu yangu Muddy O, amekuwa mwanasiasa na mwanajamii.

Nikiwa na ndugu yangu na rafiki wa siku nyingi. Mohammed Ommary, maarufu Muddy O. Nilisoma nae TSJ kuanzia cheti na diploma ya uandishi wa habari.

Tumetupana siku nyingi mpaka wiki iliyopita aliponitumia ujumbe katika simu kunambia jina lake limerudi katika nafasi mbili za uongozi wa juu wa chama cha CCM ngazi ya taifa. Nilifurahi sana aliponiambia 'kaka mimi ni mdau wako katika kidojembe'.

Kwa hivyo Muddy O atagombea nafasi ya NEC taifa na mkutano mkuu wa chama cha CCM akiwakilisha Kisarawe mkoa wa Pwani. Kwa upande wa NEC ataminyana na wajumbe 40 ili yapatikane majina 6. Mungu atamsaidia kiumbe huyu aweze kutimiza ndoto zake za siasa.

Nikiwa Rais wa chuo TSJ nilimteua kuwa waziri wangu wa masuala ya burudani na michezo, aliweza kunisaidia sana katika michezo, kadhalika nilipokuwa Mhariri mkuu wa gazeti la chuo "CHIPUKIZI' Muddy O alikuwa mwandishi wangu wa burudani na michezo. Hivyo nae ni jembe kweli kweli.

Kwa sasa amejikita sana kijijini Kisarawe, shughuli zake  sana anafanya katika taasisi ya afya katika masuala ya utafiti (NIRML). Tumezungumza mambo mengi sana na baadae tukapanga tukutane halafu nimtembelee kijijini kwake Kisarawe ili kuenda kuangalia maisha halisi ya mtanzania. Nawaahidi picha nyingi sana wiki ijayo kutoka kijijini Kisarawe.

HAFIDH A. KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
kidojembe@gmail.com
03/10/2012

No comments:

Post a Comment