mjane,Asia
Ismail ambaye ni mke wa marehemu Ismail Omary aliyeuwawa katika maandamano ya
Chadema mnamo januari 5 mwaka jana jijini Arusha akiwa amembeba mtoto wake wa
kike,Amina Ismail juzi katika mkutano wa hadhara wa Cuf uliofanyika uwanja wa
Levolosi ambapo alikishutumu Chadema kwamba kimetafuna fedha za rambirambi za
marehemu mme wake na kisha kumtekeleza pamoja na kuhaidi kumpatia.(picha na
mahmoud ahmad)
.
Mahmoud Ahmad,Arusha
MJANE,Asia Ismail ambaye ni mme wake,Ismail Omary aliuwawa katika maandamano ya januari 5 mwaka jana amekishutumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) mkoani Arusha kwamba kimetafuna fedha za rambirambi za marehemu mume wake lakini mbali na hilo pia wamemtelekeza. Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Wananchi(Cuf) uliofanyika juzi katika uwanja wa Levolosi,mjane huyo alisema kwamba Chadema walihaidi kumpatia fedha za rambirambi zilizochangwa katika uwanja wa NMC wakati wa kuaga mwili wa mme wake lakini hadi leo hajazipata. Huku akiangua kilio katika mkutano huo alisema kwamba alipewa taarifa kwamba Chadema kinachangisha fedha za rambirambi na mara watakapokamilisha mchango hiyo watampatia lakini hadi leo hajawahi kuona fedha yoyote. Mjane,huyo aliyekuwa amembeba mtoto wake wa kike jukwaani aitwaye Amina Ismail alitoa machungu hayo na kwamba fedha aliyoambulia hadi sasa ni ile iliyotolewa na kada ya CCM,Mustafa Sabodo kiasi cha sh,5 milioni . Hatahivyo,alisema kwamba mara kwa mara alikuwa akifunga safari kufika katika ofisi za Chadema wilayani hapa kwa lengo la kufuatilia fedha za rambirambi za mumewe lakini badala yake alikuwa akipigwa danadana. “Nimekuja hapa leo mkutanoni kuelezea machungu yangu ninasikitika sana kwamba Chadema ,mbali na kuchangisha fedha za rambirambi za marehemu mume wangu lakini hadi leo sijawahi kuona hata senti tano”alisema huku akinagua kilio
Hatahivyo,mjane huyo alisema kwamba pamoja na chama hicho kutangaza kuijali familia yake mara alipofariki mme wake lakini hadi leo hakuna kiongozi yoyote anayejua maendeleo ya familia hiyo. Alisema kwamba marehemu mme wake alimwachia watoto wawili ambapo kwa sasa anahangaika kuwahudumia kuwapatia mahitaji mbalimbali
No comments:
Post a Comment