Wednesday, October 3, 2012

Jk azungumzia vifo vya kinamama wa kitanzania katika ziara yake New York..


  Meya Michael Bloomberg, Ban Ki Moon, Rais  Jakaya Kikwete na Dr. Hellen wakiangalia video fupi iliyokuwa ikionyesha kazi zilizofanywa za ukoaji wa  akina mama wajawazito kwa kuwapatia huduma ya upasuaji wa dharura, huduma ambayo imepatika kwa ufadhili wa  Mameya Philanthropies Michael na Bloomberg ambapo kwa kupitia ufadhili alioufanya kuanzia mwaka 2006 zaidi ya wataalam 106 wakiwamo wakunga na manesi wamepatiwa mafunzo ya upasuaji wa dharura, pia huduma za afya zimeboreshwa kwa kujenga au kuvifanyia ukarabati vituo vya afya na zahanati katika ngazi za vijiji katika  maeneo ya  mikoa ya Pwani, Morogoro na Kigoma. Ufadhili  na kazi kubwa iliyofanywa na  Bloomberg   pamoja na juhudi za   Rais Jakaya Kikwete zimemvutia Dr. Hellen naye kuwekeza nchini Tanzania.

 Rais Jakaya Kikwete akiwa ametoklezea na katibu mkuu umoja wa mataifa Ban Ki Moon.


Rais  Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika  mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki  Moon ambaye naye aliongoza ujumbe wake. Matukio hayo yote yamefanyika siku ya  Jumanne katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  Jijini New York, Marekani.

Picha zote kwa hisani ya Mjengwa blog na Ikulu.

No comments:

Post a Comment