Monday, September 17, 2012

Bukoba hii jamani... Picha zinaanza kukubali kubali... Ila zipo nyingi sana. Msije kunidai zawadi buree, zawadi ndiyo hizo.


 Nilikwenda kutembelea chama cha waandishi wenzangu njia ya kuelekea Bukoba Club, karibu na kituo kikuu cha polisi Mkoa wa Kagera.

 Wakati nashuka ziwani nikapishana na huyu mama katika daraja akitoka kununua samaki nilijisikia furaha sana namna alivyokuwa amewabeba.

 Hii ni njia ya kuelekea Kyaka unaiacha Tanzania sasa unaelekea Uganda. Tazama uzuri wa nchi yetu...


Hili ni kanisa ambalo Cardinali Rugambwa atazikwa upya mwaka huu Octoba 6, alifariki mwaka 1997.

 Sikuwa nikijua kumbe Kagera Sugar inafuliwa na mchezaji wa zamani wa Simba Sport Club, King Abdallah Kibaden.

 Uwanja wa Kaitaba huu jamani, ndipo nyumbani kwa Kagera sugar, niliwaona wakijifua vilivyo kwa ligi kuu


 Hili ni ziwa victoria, msijekufikiri ni bahari bure. Haya tazameni maajabu ya Muumba wetu... Ziwa hili limegusa nchi tatu. Tanzania, Kenya na Uganda.

 Hizi ni moja ya athari za vita ya Kagera baina ya Tanzania na Uganda... Kanisa hili limehifadhiwa kwa kumbukumbu haruhusiwi mtu kupanda mlima huo.

Njia ya kuelekea Karagwe hii, ni Kyaka mjini hapa unaiacha njia ya kuelekea Mtukula unachepuka kushoto.

No comments:

Post a Comment