Saturday, September 15, 2012

Jana nilikutana na majembe yangu mawili chuoni... Nilifurahi kwelikweli na pia nikaenda sehemu ya makumbusho kwangu.

Hii ni Hostel ya kwanza kabisa kuishi baada ya kufika Kampala mwaka 2009 March. Leo nimeamua kuikumbuka na sitoisahau maana ilinihifadhi na kunitoa ushamba wa ugeni.
 
Kutoka kulia ni Emmanuel Makundi, tunamuita Magroup... Tulikuwa darasa moja chumba kimoja chuoni na Hostel. Naam mwana masscomm huyu, alikuwa room mate wangu hostel. ni Mbongo na kabla ya hapa tulikuwa pamoja Tanzania yeye akifanya diploma ya habari nami kadhalika ila vyuo tofauti lakini vikiwa jirani pua na mdomo Ilala Sharif Shamba. Yeye DSJ nami TSJ.

Huyu wa katikati anaitwa Evans Musoka Luseno, ni Mluya kutoka Nairobi Kenya.. Pia tulisoma nae darasa moja. Sote tupo Kampala kwa maandalizi ya Graduation 'mahafali' ya kumaliza shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma.... Hili ni eneo la chuo KIU...

No comments:

Post a Comment