Mwandishi mashuhuri wa vitabu nchini
Nigeria Chinua Achebe hatimaye amekatiza kimya chake cha miaka 40 na kuchapisha
Kitabu chake kilichosubiriwa kwa hamu na ghamu kwa jina 'There Was a Country'
yaani kulikuwepo na Nchi.
Kitabu hiki kinahusu Vita vya
Biafra vilivyodumu kwa muda wa miaka mitatu nchini Nigeria. Chinua Achebe
alihudumu kama Balozi wa kimila katika eneo zima la Biafra, pale lilipojaribu
kujitenga kutoka Nigeria mwaka 1967.
Chinua Achebe ni mmoja wa waandishi wa vitabu mashuhuri na
mkongwe zaidi barani Afrika ambaye kitabu chake cha kwanza kijulikanacho kama
"things Fall Apart" kimeuza nakala milioni 10 kufikia hivi sasa.
Kitabu hicho
kiliandikwa mwaka 1958. Kimetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 50 na kinatilia mkazo
tamaduni za jamii ya Waigbo zinavyogongana na maisha ya kizungu.
Mwandishi huyo
wa kitabu "'Birth pangs', ambaye ameshinda tuzo nyingi, ana umri wa miaka
81 hivi sasa na ameandika zaidi ya vitabu 20, vingi vikiwakosoa vikali
wanasiasa na watawala wa taifa hilo.
Chinua Achebe
anaishi nchini Marekani kufuatia ajali ya barabarani mwaka 1990. Hata hivyo
hajagusia ghasia za mauaji katika Vita vya Biafra, ambavyo vilianza akiwa na
familia yake changa. Ni mahala padogo sana anagusia vita hivyo katika mashauri
yake.
Zaidi ya watu
milioni moja waliuawa katika vita hivyo kutokana na mapigano na ukosefu wa
chakula. Picha za watoto waliokonda kutokana na njaa katika magazeti ndizo
zilizokuwa ishara ya vita vya Biafra.
Vitabu vya
Chinua Achebe, hasa kile cha Things Fall Apart kimetumiwa katika fasihi ya
Kiingereza kote katika Vyuo Vikuu na shule za upili katika Bara la Afrika na
kwingineko.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment