Wednesday, September 26, 2012

Hizi picha zinauzwa ila kwangu zinatolewa bure....

 Picha hii ilileta gumzo kubwa, kila mtu alitaka kujua hapa ni wapi. Jamani tembeeni vijijini muone maisha halisi ya mtanzania ambae tangu amezaliwa hajawai kuonja burger. Biharamulo hii wadau, asubuhi watu wakigonga kitu cha gahawaaa...

 Chato hapa kwa muheshimiwa Magufuli, Kuna mkanganyiko mkubwa sana juu ya wilaya hii nitaelezea baadae katika picha ya mbele.

 Nilipita Geita usiku, ila kamera ya jembe haina uwezo mkubwa wa kuchukua picha katika kiza. Ila nikasemalazima nibaki na kumbukumbu japo kwa picha mbaya. Shinyanga hii wadau.

 Nililala Kahama, uso umeng'aa kwa chapati za Kahama. Taaamu kwelikweli.






 Nina ugonjwa wa kupenda kusoma vitabu. Nilipofika Bukoba niliingia hapa...


 Manyoni hapa mkoa wa Singida, vijana wanapiga kazi kama hawana akili nzuri. Manyoni kuna warembo nimesikia.



 Hili ni jengo la wilaya ya Chato, nilisema nitazungumzia utata huu.Chato kwa kumbukumbu zangu ilikuwa mkoa wa Mwanza, sasa wenyeji wakwa wananichanganya mara ipo Biharamulo, mara ipo Geita mara ipo Kagera. Maana huu mgawanyo wa Mikoa na wilaya mpya umekenganya watu wengi sana.

 Huu ni mji wa dodoma,makao makuu ya Serikali barabara safi sana nilipenda kwelikweli.

 Hii ni singida mjini, napenda kuona majabali kamahayo yakiwa katikati ya mji raaaha kwelikweli.

 Jengo la bunge la Tanzania mjini Dodoma, sikulipata vuzuri ila nilitaka kubaki japo na kumbukumbu.

Njiani tukielekea Bukoba unaona vitu vizuri kama hivi, hiyo si bahari wala Ziwa,ni bwawa tu la kupendeza..

No comments:

Post a Comment