Monday, September 24, 2012

Sudan zote mbili zakubali kukaa meza moja kumaliza tofauti zao...


Marais wa Sudan na Sudan Kusini hii leo wanaendeleza mazungumzo kuhusu mizozo iliyowasababisha kukaribia kutumbukia katika vita mapema mwaka huu.
Masuala muhimu katika mkutano huo unaofanyika nchini Ethiopia ni usalama katika maeneo ya mpakani, ugavi wa mapato ya mafuta na eneo lenye utata la Abyei.
Baada ya masaa mawili ya mazungumzo siku ya Jumapili,msemaji wa serikali ya Sudan, Badr El-Din Abdallah, alisema kuwa hatua zimepigwa kati ya pande zote mbili lakini swala la amani ndilo bado linazua utata
Umoja wa mataifa umetishia kuziwekea pande zote mbili vikwazo ikiwa hazitaafikia makubaliano na amani ya kudumu
Sudan Kusini ilijipatia uhuru mwaka jana kutoka kwa Sudan baada ya makubaliano ya amani kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya zaidi ya miaka kumi.

Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment