Tuesday, September 25, 2012

Mashindayo ya kuchora kwa wanafunzi...... Kama una kipaji jitokeze.

 Mmoja wa waratibu wa shindano hilo Abdallah Chapa akitoa maelezo juu ya shindano hili katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO leo asubuhi.


 Mzee Raza ni mchoraji wa siku nyingi sana, na ana mambo mengi katika sanaa hii ya ucoraji. Jiandae kidojembe itakuja na historia yake na melezo mengine katika sanaa hii ya uchoraji nchini na afrika mashariki. Leo nilipata bahati ya kuzungumza na mzee huyu ana mambo mengi sana, nimeamua kuchukua namba zake za simu na nimeweka ahadi ya kukutana nae.... 'watch this space' ........

Mwakilishi wa baraza la sanaa Tanzania BASATA Pastori John akifafanua kitu kwa wanahabari juu ya shindano hilo.


Shindalo la Uchoraji Kwa Taasisi za Kielimu Image Profession ikishirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa mara nyingine inatangaza kuanza kwa muhula mpya wa pili wa Shindano ya Uchoraji maalumu kwa Taasisi za elimu. Shindano ambalo pia linajulikana Kama

Educational Drawing Competition au Image Profession Educational Drawing Competition, lina malengo ya kuibua vipaji katika fani ya uchoraji kwa kuzingatia uwekezaji kwa watoto na vijana. Theme/Wazo kuu la mwaka huu: ART IMITATES LIFE au SANAA HUFUATISHA MAISHA Makundi ya ushiriki  ni Chekechea, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Juu.

Shindano hili linafanyika kila mwaka na lilianza mwaka 2011. Kwa mwaka huu shindano litaanza tarehe 25 Septemba mpaka mshindi atakapotangazwa mnamo mwezi wa nne mwaka 2013.

Kwa maelezo na taratibu za Shindano tembelea Facebook Page/Group “Tanzania Drawing Competition” au wasiliana na BASATA au DRAWINGCOMPETITION – IMAGE PROFESSION, P O BOX 92 DAR ES SALAAM. SIMU:  +255 222 664 740 /  +255 713 484 040 /   class="skype_pnh_logo_img" v:shapes="_x0000_i1027">+255 714 676 217 /  +255 716 430 084 EMAIL: info@imageprofession.com

No comments:

Post a Comment