Wednesday, September 26, 2012

Leo JK alifanya kazi za jeshi tu... Siku nzima.

  Amiri jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam.

 JK akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa juu wa jeshi pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam..

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda (kulia). Picha zote na Aron Msigwa- MAELEZO.
 

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  pole kwa ndugu wa Meja Jenerali Mstaafu  Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU

Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment