Thursday, September 27, 2012

John Terry kukosa mechi nne na kulimwa fidia ya Pauni 220,000 za Uingereza kwa kosa la utovu wa nidhani uliofananishwa na ubaguzi wa rangi dhidi ya wtu weusi katika soka.


John Terry ameadhibiwa na chama cha kandanda cha England, FA, asicheze mechi nne, na vile vile alipe faini ya pauni 220,000, kutokana na matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand. 

Chama cha FA kilithibitisha Terry alifanya makosa hayo, baada ya kusikiliza kesi dhidi yake kwa kipindi cha siku nne. 

Msemaji wa John Terry alisema mchezaji huyo "alisikitishwa" na hatua ya FA, kwa kuamua tofauti, kinyume na mahakama, ambayo awali ilisema hana makosa. 

Mwezi Julai, mahakama ya Westminster mjini London ilipitisha uamuzi kwamba mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 31, hakufanya kosa hilo, la kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Ferdinand. 

Hata hivyo wengi watajiuliza kwa nini adhabu dhidi ya Terry ni nyepesi mno, ikilinganishwa na ile iliyopitishwa dhdi ya mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez mwaka jana. 

Terry ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, mara tu atakapopokea maelezo ya adhabu hiyo kupitia maandishi. 

Adhabu hiyo haitatekelezwa hadi Terry atakapopata nafasi ya kuamua atafanya nini. 

Taarifa kutoka klabu yake ya Chelsea iliongezea: "Klabu ya Chelsea inafahamu vyema uamuzi uliopitishwa, na inaheshimu uamuzi huo uliotolewa leo na chama cha FA kumhusu John Terry."

Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment