Wednesday, September 26, 2012

Zawadi za picha zinazidi kufunguliwa, usipitwe tafadhali...

 Gari imebeba gari, mizani ya Mikese hii mjini Morogoro... Hivi barabara zitapona kwa hali hii?

 Gairo hapa, kuna hoteli nzuri kwelikweli. Ila nikajiuliza swali kwanini wanavijiji hawafaidiki na ajira za miradi mikubwa kama hii? Matokeo yake hata wahudumu wanatoka mijini. Wanavijiji wanaishia kuuza vikaranga na matunda...
 Hii ndiyo Tanzania... Ukiimba ule wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka. Unazungumzia maeneo kama haya. Ila watanzania wengi hawataki kuja kutembelea kutazama mandhari nzuri na za kuvutia za nchi yetu. Matokeo yake wageni wanajua zaidi vijiji vyetu na vivutio kuliko sisi wazawa. Morogoro hii safu za milima ya uluguru.




 Hizo picha za juu zote ni kituo kikuu cha mabasi Morogoro mjini- Msamvu hapa. Na hiyo Hoteli nilifanikiwa kulala mwaka 2008 ikiwa haijamaliziwa. Nilikuwa na shemeji yenu mama yake mtoto, tulifaidije?

 Tazama hizo nyumba, huoni kitu chochote cha kuleta faraja. Hakuna bomba la maji wala nguzo ya umeme. Na paa limezuiliwa na mawe badala ya misumari. Ikija mvua ya tufani je?


Hii ndiyo Tanzania na watanznia takriban asilimia 80 wanaishi vijijini. Serikali ina mpango gani nao?

No comments:

Post a Comment