Friday, September 28, 2012

Mshindi wangu Dada Bertha Charles leo alikuja kunitembelea jembe lenu nyumbani Tandale kwa mtogole mtaa wa mkunduge kwa mfuga mbwa aka kwa mafundi simu.

                                  Hapa akionekana kufurahia kufika kwa kaka yake jembeeeee...

Akiwa ametoklezea na jembe baada ya kufanyiwa interview bila ya kujijua. Si unajua tumepikwa katika fani hii ya uandishi?

Kuanzia sasa nimepunguza ama kuacha kushabikia shindano la kusaka vipaji Tanzania la BSS, sina ugomvi na shindano hilo wala waandaaji. Sababu ya msingi ni kuwa mshindi wangu ametangulia kutolewa.

Leo dada Bertha ambae alikuwa ni mshiriki akiwakilisha jiji la maraha la Dar es Salaam aliamua kunitafuta kaka yake, nikamuelekeza nyumbani na nashukuru hakupotea. Nilizungumza nae mambo mengi sana, lakini nilijitahidi kumuonyesha kuwa kila kitu kipo sawa ingawa moyoni kwangu haikuwa hivyo.

Aliposhuka kwenye 'bajaj' ama tuktuk, kama kawaida yake alianza kuniita jina langu kwa kwikwi kama mtu aliekuwa akitaka kulia. Lakini nikamkumbatia na kumminya mwili wake ishara ya kumuonyesha upendo na kumwambia 'every thing is okey, there is life even outside the BSS' Nashukuru alielewa na kuyarudisha nyuma machozi yake. Namjua kwa kupenda kulia.

Nilipanga nikionana nae nimuhoji baadhi ya maswali halafu niandike chochote ndani ya kidojembe, ila sikutaka ajue chochote kinachoendelea. Najua kwa sasa hapendi vyombo vya habari ila amesahau kama kaka yake ni miongoni mwao. (So this is a surprise to you Bertha)

Alinambia wale washiriki wote walikuwa ni wa kawaida sana na kilichomfanya atoke mapema mpaka sasa hajui ni kitu gani. Hata baadhi ya wakufunzi na washiriki wenzie hawajui ni kitu gani kilitokea siku ile alipotajwa jina lake.

Cha ajabu nilipomdadisi zaidi ili kujua kama anahuzunika kwa kutolewa kwake, alinijibu "Kimsingi kido mimi sijutii kutoka, najihisi kama kuna kitu kimepungua ndani ya mwili wangu baada ya kutoka, hata 'crue' (watu waliokuwa wakichukua picha) ilishangaa sikulia wala sikucheka. Hakika nilikuwa katika wakati mgumu sana, si kwa ubaya but i feel like i'm free," alisema Bertha.

Baada ya BSS maisha yanakwendaje mtaani: "Nimeamua nikafanye ngoma katika moja ya nchi hizi tatu za Afrika Mashariki, Bongo, Kenya ama Uganda. Na aliendelea kufafanua kuwa akiitwa katika tamasha la top 20 mwisho wa shindano la BSS atakuwa na ngoma yake ambayo kwa wakati huo itakuwa hit mbayaaa... lakini nataka nikafanye ngoma kali ambayo itawaonyesha mashabiki wangu kuwa naweza na kushiriki BSS ilikuwa ni kutaka kupata njia na nashukuru sana BSS imenisaidia kunikutanisha na watu wengi.

"Nimeweza kufunzwa mambo mengi juu ya muziki ambayo sikuwa nikiyajua na sasa ninatambua aina za uimbaji na hata Chief Judge Madam Rita ametuambia washiriki wote tukiwa na shida ya aina yoyote tumuone atatusaidia," alisisitiza Bertha.

Swali la kizushi kwake ilikuwa ni uhusiano wake na judge matata wa BSS Salama Jabir, "Huwezi amini yule dada ananikubali sana tofauti na watu wanavyoona kwenye TV. Mwanzo niliona kama ananichukia lakini ni mshikaji ile mbaya."

baada ya kuzungumza nae sana niliamua kumsindikiza mpaka kwao na jembe kurudi uswahilini kwetu.

Bertha Charles wewe ndie uliekuwa ukinifanya nitazame BSS na sasa sioni hiyo sababu. Kwa hakika tulikuwa na mipango mingi sana kwa dada huyu, nilimweleza namna wanafunzi Uganda walivyokuwa wakimpenda mpaka kwenye facebook Page ya Epic BSS yeye ndie aliekuwa akiongoza kwa 'likes' wengine mhh.....

Na hata uamuzi wa kutengeneza facebook page yake ambayo tayari nishaanza kuiandaa na picha nishakusanya tangu za shindano la KIU Star Search lililofanyika mwaka 2008 chuoni KIU Kampala. Aliposikia hivyo macho yake yalianza kung'aa nikajua anataka kulia. Nikaanza kumchekesha ili kumsahaulisha. Ila najua anaumia na alikuwa akirudia neno hili la kizungu ambalo lilikuwa likinikera sana 'i'm sorry i know i have disappointed you guys'.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
kidojembe@gmail.com
0713 593894/ 0752 593894
28/09/2012

No comments:

Post a Comment