Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania alikuwa nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu akitokea nchini Uganda aliposhiriki mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Kongo. JK amefanya ziara yake rasmi ya kwanza nchini Kenya tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2005. Ingawa alikuwa akienda nchini Kenya kwa shughuli za hapa na pale, lakini hii ya juzi ndiyo ziara yake rasmi nchini humo.
Hapa alitembelea
Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya
(KARI)
JK akipanda mti wa kumbukumbu mara alipozuru mtambo wa
kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke utokao chini ya ardhi wakati wa Ziara Rasmi
ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini Kenya.
Rais Kikwete alipotembelea shamba la kondoo wa kisasa katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi.
No comments:
Post a Comment