Ufaransa imesema itafunga kwa muda balozi na shule
zake katika nchi 20 siku ya Ijumaa baada ya gazeti moja nchini humo
kuchapishwa vibonzo vinavyomkejeli Mtume Muhammad.
Hatua ambayo inahofiwa huenda ikazidisha wasiwasi nchini humo siku ya Ijumaa.Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema ana wasiwasi na picha 20 zilizochapishwa katika gazeti la kejeli la kila wiki (Charlie Hebdo) ambalo liliyafanyia mzaha maandamano ya hivi karibuni ya kupinga filamu ya Marekani inayomkejeli Mtume Muhammad.
Amesema huenda uchapishaji wa vibonzo hivyo ukazidisha hali ambayo tayari inatokota katika nchi za kiisilamu.
Vikaragosi hivyo vinaonekana vikikejeli waisilamu waliozua ghasia wiki jana kupinga filamu iliyonuiwa kudhihaki uisilamu.
Bwana Fabius alisema kuwa mikakati mingine zaidi ya usalama itaweza kuchukuliwa katika balozi za Ufaransa kote duniani.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment