Monday, September 24, 2012

Leo jembe nilikuwa katika 'Round table meeting' katika jengo la kituo cha sheria kujadili upatikanaji wa gas na oil... Tanzania.

 Kutoka kushoto ni mkurugenzi wa sera na utafiti Hakielimu Godfrey Boniventure, wa pili ni Irenei Kiria mkurugenzi wa SIKIKA na wa mwisho ni mwanadada Gloria magole afisa wa ufuatiliaji kazi za serikali kituo cha sheria na haki za binaadamu Tanzania.


 Hata said Kubenea pia alikuwepo wa kwanza kutoka kushoto, alituchekesha wakati akijitambulisha 'Mimi naitwa Said Kubenea ni mwanahabari ila sina chombo chochote' ahahaaa. Said Kubenea ni mwandishi wa habari za uchunguzi ambae gazeti lakeMwanahalisi  lilifungiwa mwezi uliopita kwa kuandika habari kuwa Serikali ilihusika katika kushambuliwa mwenyekiti wa madaktari Dk Steven Ulimboka.

Wanahabari hao wakifuatilia kwa makini mazungumzo juu ya mustakabali wa gesi asilia nchini mwao Tanzania.

Subirini Habari kamili bado naipika, inaweza kutoka kwenye gazeti la Raia Mwema Jumatano hii, hivyo itakapotoka tu nitaiweka humu nanyi mfaudu....

No comments:

Post a Comment