Thursday, September 27, 2012

Hii katika pitapita zangu katika blogs za wenzangu nikaikuta. Kwakuwa kidojembe ni blog ya kijamii nikaamua kuirusha ili wadau wengine watoe michango kama ikiwezekana. mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com unaendelea kuwashukuru wote wanaoendelea kutoa michango yao kunusuru uhai wa mtoto Juliana ambaye ni yatima

Mtandao huo unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin
Tunaombwa kuungana pamoja kwa ajili ya  kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidiNo comments:

Post a Comment