Monday, September 24, 2012

Zawadi zenu hizi naanza kuzifungua kidogokidogo.....

 Jamani hii ni Gairo mji mdogo kuelekea Dodoma.... bidhaa za jikoni bei nzuuuuriii.......

                Gairo Chips ndiyo ghali, tazama hicho kifuko kina chips na nyama ati 3000...

                           Ukitaka Zabibu nenda Dodoma wala usihangaike utaibiwa bure....

                                     Shinyanga hii jamani niliingia usiku..... Mji wa Kahama huu...

                                      Biharamulo hii asubuhi......

 Wakati narudi nilifurahi sana baada ya kuona ardhi ya kwetu baada ya kuiacha kwa wiki mbili. Namanga hii mpaka wa Kenya na Tanzania.

 Moshi ipo mkoa wa Kilimanjaro, inasadikiwa ndiwo mji msafi kuliko yote afrika ya Mashariki. Unachuana na Kigali nchini Rwanda.


 Hii ni njia panda ya Himo, ukitoka Dar es Salaam kulia unakwenda Holili mpaka wa Kenya na Tanzania, kushoto unakwenda Moshi... sasa niliona hili tangazo la kupigia kura vivutio vya taifa. Nikajiuliza hao watu waliokaa hapo chini wanajua maana ya tangazo hilo, na je wameshapiga kura?

 Mwanga hii Mkoa wa Kilimanjaro, eneo hili ni kame sana, jua kali na watu hupenda kukaa chini ya miti. Na nimesikia kwenye maeneo ya jua kali nyoka hupenda kukaa kwenye miti kufuata kivuli... Mhhhh!!!!??

 Hapa ni kijiji cha Kisangara, wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro. Hivi mkonge wetu umepotezaje thamani?

 Jamani hii ni Wilaya ya Mombo kijiji cha Mazinde Mkoani Tanga.... Watu hawa wanajua kama kuna facebook?

Mombo hii.... kama kawaida nilinunua furushi la mbogamboga kwa 8000 tu.... mjini kwa pesa hiyo utaambulia kapu nusu....

picha bado zipo nyingi na nitaendelea kuzitoa kwa lengo la kuelimisha, kujuza, kuburudisha na kuasa. Naam picha zinazungumza maneno 1000 na uzuri ni kuwa hata kama hujui kiswahili picha inazungumza lugha yoyote...

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
kidojembe@gmail.com
25/09/2012

No comments:

Post a Comment