Chelsea imekuwa timu ya kwanza kuichapa
Arsenal katika mechi za ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuwachapa 1-2
katika uwanja wao wa nyumbani,Emirates siku ya Jumamosi.
Vijana wa Roberto Di Matteo
ndio walikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 20 kupitia mshambulizi
Fernando Torres baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Juan Mata.
Lakini katika dakika ya 42 mshambulizi Gervinho alifunga bao safi hivyo kuzifanya timu
hizo mbili ziende mapumzikoni zikiwa sare ya 1-1.
Na katika dakika
ya 52 ya kipindi cha pili, Mata alipiga mkwaju mwengine wa adhabu ambapo
ulimshinda mlinzi Laurent Koscielny na badala yake kumgonga mguu na kuingia
ndani huku ikimuacha Kiper wa Arsenal Vito Mannone hoi.
Wenger amekua
akilalamika kwamba safu yake ya nyuma imekuwa ikizembea katika mipira ya
adhabu.
Licha ya
kufungwa huko, Arsenal walitawala ngoma hiyo nzima ya Jumamosi lakini safu ya
mbele ya vijana hao wa Arsene Wenger iliyonekana kukosa makali na kuwa na
kukosa umakini.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment