Sudan na Sudan Kusini zimetia saini
makubaliano kuhusu biashara, mafuta na usalama ingawa hazijakubaliana kuhusu
mipaka.
Baada ya mazungumzo ya siku ya
nne, nchi hizo mbili zimeafikiana kuruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka kusini
kupitia mabomba ya Kaskazini na kuondoa wanajeshi mpakani.
Viongozi wa nchi hizo mbili hatimaye wamekubaliana baada ya
mazungumzo ya siku nne mjini Addis Ababa Ethiopia .
Lakini maswala
kadhaa muhimu bado kutatuliwa ikiwemo kuafikia makubaliano kuhusu mipaka
inayozozaniwa ikiwa ni mojawpao ya kilichosababisha mgogoro ambao nusura
utumbukize nchi hizo kwenye vita mapema mwaka huu.
Baada ya mapigano
kuzuka kuhusu mzozo wa mafuta na mipaka, Umoja wa mataifa ulitishia kuziwekea
pande zote mbili vikwazo ikiwa hazitaafikia makubaliano ya kina.
Wapatanishi wa
Muungano wa Afrika wangali kuthibitisha kuwa makubaliano yameafikiwa lakini
rais wa Sudan Omar al-Bashir na mwenzake wa Kusini Salva Kiir, wanatarajiwa
kutia saini makubaliano hayo hii leo.
Maelezo
yametolewa tu kwa mukhtasari lakini wapatanishi wa pande zote mbili, walisema
kuwa wamekubaliana kuhusu eneo la nchi hizo mbili ambalo halina ulinzi wa
kijeshi.
Pia makubaliano
ya kiuchumi yaliafikiwa kuruhusu Sudan Kusini kuanza tena shughuli zake za
kuzalisha mafuta.
Lakini mwafaka
haukupatikana kuhusu eneo linalozozaniwa la Abyei wala mipaka mingine mingi
ambayo nchi hizo zinazozania.
Kwa hivyo
makubalino hayo hayajaweza kutimiza masharti ya Umoja wa Mataifa kwa nchi hizo
kuafikia mkataba unaotatua mzozo huo kwa kina.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment