Uwanja wa nyumbani huu Mkwakwani mjini Tanga Kocha mkuu wa Wagosi wa kaya Juma Mgunda akiwajibika.
Hii ilikuwa ni mechi ya kirafiki Coastal na Yanga iliyochezwa katika uwanja mpya wa Taifa. Ambapo Coastal ililala 2-1...... Siku ya pili Coastal ilicheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Chamanzi ambapo Coastal ililala 2-0.
''kwa mapenzi makubwa niliyo nayo juu ya timu yangu ya Coastal
Union nimeamua kujiuzulu kufundisha Coastal union ili itimize malengo yake
iliyojipangia ikiwa na amani na utulivu.......Mungu ibariki Coastal
Union''................Maneno ya Juma Mgunda baada ya kuchukua maamuzi magumu
ya kujiuzulu leo asubuhi.
Hii ndiyo habari yenyewe niliyoipata, lakini baada ya kuwapigia simu wadau na mashabiki waliopo Tanga walisema habari hizo zipo lakini bado Juma Mgunda hajazungumza rasmi na vyombo vya habari.
Lakini imeshathibitishwa kuwa katika mechi ya kesho ya ligi kuu katika uwanja wa nyumbani ambapo Coastal itakutana na Kagera sugar inayonolewa na mkongwe wa siku nyingi wa Simba King Abdalaah Kibaden, Juma Mgunda hatokuwepo katika benchi la ufundi badala yake benchi litaongozwa na kocha wa makipa mkongwe Juma Pondamali Mensah.
Mpaka sasa Coastal Union imeshacheza mechi tatu moja ugeninii na mbili nyumbani. Imeshinda mechi moja ya nyumbani dhidi ya Mgambo FC ya mjini Tanga iliyopanda daraja msimu huu, mechi nyingine ilikuwa ni dhidi ya Toto Africa na ya tatu ilikuwa ya ugenini dhidi ya Prison mjini Mbeya ambapo ilitoa suluhu mechi zote mbili.
Fuatilia kidojembe kesho ili kama kuna taarifa zozote mpya kuhusiana na hatma ya Juma Mgunda ambae ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union katika safu ya ushambuliaji......
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
kidojembe@gmail.com
0713 593894/ 0752 593894
25/09/2012
No comments:
Post a Comment