Wednesday, September 19, 2012

Jembe Lema kusuka au kunyoa leo...

Aliekuwa mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya chadema Godbless Lema, ambae alivuliwa ubunge na mahakama ya Arusha miezi kadhaa iliyopita kwa kile kilichoelezwa ni kuharibu uchaguzi uliomuweka madarakani leo rufaa yake itaanza kusikilizwa.

Lema ambae alituhumiwa kutumia mbinu chafu za kumchafua mpinzani wake Dk Batilda Buriani (CCM) ambae sasa ni balozi wa Tanzania nchini Kenya, alifutwa ubunge wake na mahakama kuu mjini Arusha baada ya kuonekana utetezi wake ni dhaifu na haukuwa na mashiko.

Dk Batilda Buriani, ambae alikuwa anagombea kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini alifungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo kwa madai alidhalilishwa kwa kuitwa mfuasi wa chama cha kigaidi duniani Al-Kaeda kwa kuwa alikuwa akivaa kilemba.

Aidha Dk Buriani aliendelea kuel;eza kuwa alitolewa maneno ya udhalilishaji kama kudaiwa kuolewa na muislamu anaeishi mjini Zanzibar huku yeye akijiita ni muumini wa dini ya kikristo. Hayo na mengine mengi yalitosha kumridhisha hgakimu wa mahakama ya Arusha na kumvua ubunge ndugu Lema ambae alionekana kupendwa na wengi.

Hata hivyo kwa muda wote ambao kesi ilikuwa ikiendelea Dk Buriani hakuonekana mahakamani zaidi ya kuwakilishwa na mawakili wake na jamaa wa karibu. Hiyo ilitokana na kukosa matumaini ya kushinda kesi hiyo na kadhalika kuteuliwa na Raqis Kikwete kuwa mwakilishi wa Tanzania nchini Kenya ambapo mpaka sasa anafanya kazi hiyo.

Hebu leo tutege sikio kuona labda rufaa ya Jembe Lema inaweza kuzaa matunda ama hakimu ataitupilia mbali. Na ikiwa atashinda labda cheche zake bungeni zitarudi kuwawakia Mawaziri wa Serikali ya JK.

HAFIDH KIDO
KAMPALA, UGANDA  


No comments:

Post a Comment