Tuesday, September 25, 2012

Kidojembe inaungana na wanahabari wote kutoa pole kutokana na msiba wa mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima.... dada Agness....


Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Agness Yamo (pichani) amefariki dunia. 

Habari zilizotufikia katika meza yetu ya Fadher Kidevu Blog zinasema Agness Yamo amefariki leo Sept 25, 2012 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kakayake Buguruni Sokoni katika Magorofa ya Muhimbili. Marehemu alizaliwa 8/8/1978 na katika uhai wake alifanya kazi katika makampuni mbalimbali ya magazeti na hadi mauti yanamfika alikuwa Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima. 

Bwana ametoa na bwana ametwaa, Jina la Mungu lihimidiwe….

Chanzo FatherKidevu blog

No comments:

Post a Comment