Sunday, September 16, 2012

CCM yafanya mambo uchaguzi mdogo Bububu...


Hussein Makungu alievaa kofia, akinyanyuliwa mkono na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar balozi Seif Idd, kuashiria ushindi.

Chama cha Mapinduzi kimeshinda katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika leo katika Jimbo la Bububu kutokana na kifo cha aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Salim Amour Mtondoo.

Akitangaza matokeo Misimaamizi wa Uchaguzi huo Suluhu Ali Rashid amesema kuwa Hussein Ibrahim Makungu wa CCM ameshinda kwa kupata kura 3371 sawa sawa na asilimia 50.7ambapo Issa Khamis Issa wa CUF amepata kura 3204 sawa sawa na asilimia 48.2

Aidha Suluhu amesema kuwa Mgombea wa Chama cha ADC Zuhura Bakari Mohamed amepata kura 45 sawa sawa na asilimia 0.7 wakati Abubakar Hamad Said wa Chama cha AFP amepata kura 8 sawa sawa na asilimia 0.1, Mtumweni Jabir Seif wa Jahazi Asilia amepata kura 7 sawa sawa na asilimia 0.1,Haroun Abdulla Said wa NCCR amepata kura 3 sawa sawa na asilimia 0.0, Suleiman M.Abdulla wa NRA amepata kura 1 sawa sawa na asilimia 0.0 Seif Salim Seif amepata kura tatu sawa sawa na asilimia 0.0 na Juma Metu Domo wa Chama cha SAU amepata kura 4 sawa sawa na asilimia 0.1.

Jumla ya kura 6720 zilipigwa sawa sawa na asilimia 68.6.Kura 74 ziliharibika sawa sawa na asilimia 1.1Kura halali ziliozopigwa zilikuwa 6646 sawa sawa na asilimia 98.9na waliojiandikisha walikuwa 9799.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR16/9/2012

No comments:

Post a Comment