Saturday, September 15, 2012

Maalim Seif ziarani London..Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi ya balozi wa Tanzania nchini Uingereza, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo juzi. pembeni yake ni balozi wa Tanzania nchini Uingereza balozi Peter Kallaghe.


Maalim Seif, aliwasili London, Uingereza juzi usiku (Jumanne, 11 Septemba 2012) kwa ziara ya siku nne akitokea Marekani alikokwenda kuhudhuria Mkutano wa Democratic Party, kwa mwaliko rasmi wa chama hicho. Maalim Seif jana (Jumatano, 12 Septemba 2012) alitembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo hapa London na kuzungumza na Maafisa wa Ubalozi huo na baadae kula nao chakula cha mchana. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar leo asubuhi amekutana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Uingereza, Mheshimiwa Mark Simmonds na mchana huu anakutana na mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waliopo hapa London. Kesho Mheshimiwa Maalim Seif anatarajiwa kukutana na Watanzania wote walioko London katika sehemu itakayotangazwa hapo baadae, kabla ya kuanza safari ya kurejea Tanzania leo Jumamosi asubuhi.

Picha na habariMr. A. Rashid Dilunga

No comments:

Post a Comment