Saturday, September 15, 2012

Maisha Plus inazidi kupasua anga...



 Katika hii timu kuna majembe yangu mawili hapa, Msafiri Shaaban, wa kwanza kushoto waliochuchumaa fulana nyeusi na Samira Kiango, wa kwanza waliosomama kutoka kulia mwenye rasta ama dread locks... Nilikuwa nao TSJ.



Baada ya kukamilisha usaili Dodoma, Kahama, Kagera,Singida, Mwanza, Morogoro, Iringa sasa usaili unaelekea mkoani Mbeya ambapo utafanyika Sept 15 .

Crew nzima ya Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula inayodhaminiwa na banki ya NMB na Oxfam baada ya hapo itaendelea na safari kutoka Mbeya moja kwa moja mpaka Kilwa, ambapo itafanya usaili Septemba 17, kesho yake yaani Septemba 18 usaili utaelekea Masasi mkoani Mtwara.


Septemba 20 itakuwa zamu ya Wanzanzibar kusailiwa katika kumpata mwakilishi wa Maisha Plus kisha timu itarejea Dar tayari kwa usaili ambao utafanyika Septemba 22 na 23.


Kitakachofuata baada ya usaili wa Dar ni kipindi cha Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula kuanza kuonekana kwenye runinga yako. Usikae mbali na TBC1 kwasababu ndiyo itakayokusafirisha nchi nzima ukiwa kwenye sofa lako nyumbani.


Kubwa kuliko


Wakati usaili ukiendelea mikoani nchini, Huko nchini Burundi nako usaili wa kuwapata washiriki wawili ulikuwa unafanyika kwa maana hiyo safari hii shindano la Maisha Plus litakuwa na washiriki kutoka huko.


Huu ni mwanzo wa shindano hili wa kuzishirikisha nchi zote za Ukanda wa Mashariki ya Afrika.


Kwa wakazi wa Dar fomu za ushiriki zinapatikana katika duka la Masoud Kipanya lililopo Millenium Tower, Kijitionyama. Unaweza kupata usaidizi ka kupiga namba hii 0717 710303.

No comments:

Post a Comment